23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WAZUNGU WAGUNDUA MBINU ZA KUTAMBUA KINACHOMLIZA MTOTO

Na JUSTIN DAMIAN


WATAFITI nchini Taiwan wamegundua teknolojia mpya yenye uwezo wa kutambua sababu za mtoto mchanga kulia.

Teknolojia hiyo inaitwa Infant Cries Translator imegunduliwa katika chuo kikuu pamoja na Hospitali ya Taifa ya Taiwan. Pamoja na mambo mengine, teknalojia hiyo ina uwezo wa kutofautisha aina nne tofauti za sauti anazotoa mtoto anapolia kwa kuzirekodi na kuzilinganisha na sauti zilizohifadhiwa kwenye kumbu kumbu.

Katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili, watafiti walikusanya sauti za vilio 20,000  kutoka kwa takribani watoto wachanga 100 na kuziweka kwenye sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu (online data base). Tofauti kati ya sauti hizo iliwawezesha watafiti hao wakiongozwa na Dk. Chen Si-da kuweza kotofautisha milio ya sauti hizo.

Kupitia teknolojia hiyo, mtu anaweza kufahamu mtoto analia kwa sababu gani ndani ya dakika 15 kupitia simu yake ya mkononi ambayo huwekewa teknolojia hiyo. Watafiti wanasema ufanisi wake ni asilimia 92 kwa watoto wa chini ya wiki mbili na huwasaidia kuwafahamisha wazazi kujua iwapo mtoto ana njaa, usingizi maumivu au amekojoa. Hata hivyo, ufanisi hushuka kadiri umri wa mtoto unavyoongezeka.

“Infant Cries Translator ina uwezo wa kutofautisha aina nne tofauti za sauti pindi mtoto anapolia. Unaweza kugundua kama ana njaa, usingizi, maumivu au amelowana na mkojo. Mrejesho kutoka kwa watumiaji unaonyesha kuwa ufanisi ni asilimia 92 kwa watoto wa umri chini ya wiki mbili. Kwa watoto chini ya mwezi mmoja au miwili, ufanisi ni asilimia 84 au 85 huku kwa mtoto wa miezi minne ufanisi ukiwa ni asilimia 77,” anasema Chuan-yu.

Watengenezaji wa teknolojia hiyo wanasema hakuna sababu za msingi za kuitumia mtoto anapofikia umri wa miezi sita kwa kuwa tayari anakuwa ameshazoea mazingira lakini wanaamini kuwa ni nyenzo muhimu kwa wazazi wanaopata watoto kwa mara ya kwanza.

“Baada ya kuiweka kwenye simu ya mzazi, tunaweka tarehe ya kuzaliwa ya mtoto pamoja na utaifa wake. Mtoto anapolia tunabonyeza sehemu ya simu kurekodi kwa dakika kumi na sauti hiyo itachukuliwa na kuwekwa kwenye simu. Baada ya kuhifahiwa teknolojia itafanya kazi yake kwa kufanya uchambuzi na mwisho itatambua sauti hiyo ambapo majibu hurudishwa kwenye simu ya mzazi. Mzazi ataangalia majibu na kuona ni ya kweli kabla ya kuamua hatua ya kuchukua,” anasema

Guo Young-ming, ambaye ni baba wa miaka 41 alianza kutumia teknolojia hiyo Desemba mwaka jana, siku nne baada ya binti yake kuzaliwa.

“Kwa wazazi kama sisi ambao tunapata mtoto kwa mara ya kwanza, tunaogopa mno tukiona mtoto analia kwa sababu mara nyingi huwa hatujui tufanye nini. Tunapokuwa hatuji tufanye nini teknolojia hii inakuwa msaada mkubwa kwani ndiyo hutuambia tuchukue hatua gani baada ya kutueleza tatizo linalomfanya mtoto alie,” anasema.

Chen ambaye ni daktari bingwa wa watoto, anasema wakati watoto wachanga wanasikia njaa wanatoa sauti inayoitwa Sucking Reflex. Midomo yao inakuwa ikizunguka huku na kule na mara nyingi ulimi wao hulamba midomo na huangaika kutafuta ziwa la mama ili anyonye. Kwa maana hii, tunaweza kuelewa kuwa mtoto ana njaa anapofanya vitendo kama hivi, lakini kama atakuwa ana maumivu pengine inaweza kuwa vigumu kujua kinachowasumbua na hapa teknolojia hii inaweza kuwa ya msaada kwa kuwa katika kama hali kama hii unahitaji daktari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles