25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa zamani wa Ecuador achaguliwa kuwa Rais Baraza Kuu la UN

Mwandishi Wetu, Marekani



Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje nchini Ecuador, Maria Espinosa amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Baraza Kuu la 73 la Umoja wa Mataifa akiwa ni mwanamke wanne kushikilia nafasi hiyo na mwanamke wa kwanza kutoka Amerika ya kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari hapa katika Makao Makuu wa Umoja wa Mataifa amesema katika vipaumbele vya utendaji wake ni Tekeleza, Wajibika, Husisha, Ufanisi (DARE).

Mkutano huo umezinduliwa rasmi jana huku viongozi na wakuu wanchi 193 wamethibishwa kuwa kushiriki na Tanzania itawakilishwa na kiongozi wa ngazi ya juu ambaye bado hajatajwa na anatarajiwa kutoa hotuba yake siku ya Alhamisi mchana.

Mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa hufanyika kila mwaka ambako wakuu wa nchi wanachama Tanzania ikiwamo wanapata nafasi ya kukutana na kujadili Agenda ya msingi na eneo maalumu wanalotarajia kutilia mkazo na katika mkutano wa mwaka huu ni majadiliano kuhusu hatua zinachochukuliwa kumaliza ugonjwa wa kifua kikuu, masuala ya wakimbizi pamoja na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo hata serikali ya Tanzania na jumuiya mbalimbali za kimataifa zimeanza kulipa uzito jambo hilo linalogharimu maisha ya watu kutokana na magonjwa hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles