23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri wa Ulinzi Israel ajiuzulu

JERUSALEM, ISRAEL



WAZIRI wa Ulinzi nchini hapa, Avigdor Lieberman amejiuzulu kufuatia uamuzi wa Baraza la Mawazri kukubali kusitishwa mapigano yaliyodumu kwa siku mbili katika ukanda wa Gaza dhidi ya wapiganaji wa Palestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza – BBC, Lieberman ameishutumu hatua hiyo na kuiita kama ni kusalimu amri kwa ugaidi.

Alisema chama chake cha mrengo wa kulia cha Yisrael Beiteinu kinaweza kujitoa katika Serikali ya mseto, hali ambayo inaweza kusababisha uchaguzi wa mapema.

Watu wanane waliuawa siku ya Jumatatu na Jumanne wapiganaji walipofyatua roketi 460 kuelekea upande wa Israel na majeshi ya Isreal nayo yakishambulia kwa mabomu Gaza.

Usimamishaji wa mapigano kwa kiasi kikubwa ulifanyika siku ya Jumatano, huku shule na shughuli za kibiashara kusini mwa nchi zikifunguliwa tena, baada ya kutoripotiwa mashambulizi ya roketi usiku mzima.

Hata hivyo wanajeshi wa hapa walisema wamempiga risasi na kumkamata Mpalestina mmoja ambaye alikuwa akijaribu kuvunja waya ambao ni mpaka kati ya Israel na Gaza wakati akitaka kurusha mlipuko.

Maofisa wa afya wa Kipalestina wameripoti pia kuuawa kwa mvuvi mmoja, baada ya kushambuliwa na askari wa Israel kaskazini mwa Gaza.

Wanajeshi hao walisema wamemshambulia kwa sababu alikuwa akielekea kwenye waya ulioko mpakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles