30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri: Taasisi zitakazosambaza KY kufungiwa

kyjely

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambayo yatabainika  yanaendelea   kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, yatafutiwa usajili.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa ‘facebook’.

Alisisitiza kuwa serikali italisimamia suala hilo kwa ukamilifu.

“Sijapiga marufuku matumizi ya vilainishi, ukweli nimepiga marufuku mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kununua na kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanaume wenzao na sababu nimeshazieleza,” aliandika na kuongeza:

“Na nafurahi kuwajulisha kuwa tayari baadhi ya mashirika hayo yameanza kutekeleza agizo hili kwa   kuondoa vilainishi kwenye miradi yao. Nayapongeza sana. Niendelee kuyataka mashirika mengine kutii agizo hili ambalo tutalisimamia kwa ukamilifu.

“Serikali haitasita kuchukua hatua ikiwamo kuyafutia usajili mashirika yanayoendelea na miradi ya kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja”.

Aliyataka mashirika hayo kushirikiana na serikali kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kujikita kwenye afya nyingine  inayozingatia sheria za nchi  na mila na desturi za Watanzania.

Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, Waziri Ummy alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini matumizi ya vilainishi hivyo yanachochea kuongezeka  vitendo vya ushoga ambavyo ni kinyume na sheria za nchi.

“Lengo pia ni kudhibiti maambukizi ya VVU kwa sababu katika   wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, asilimia 23 tayari wana maambukizi hayo.

“Tumebaini baadhi ya wadau wanaotekelezeka shughuli za makundi maalum wamekuwa wakikiuka taratibu za  utendaji na kusambaza vilainishi hivyo.

Awali agizo hilo lilizua mjadala mkubwa katika mitandao ya  jamii, wengi wakikosoa uamuzi huo wa Serikali kupiga marufuku vilainishi hivyo.

Walisema  kwamba vinatumika katika mambo mengine mtambuka hususan hospitalini huku wengine wakisema viendo vya ushoga havichangiwi na kuwapo   vilanishi bali ni mmomonyoko wa maadili uliotamalaki nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles