30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu wa Iraq kujiuzulu baada ya watu kupoteza maisha

BAGHDAD, IRAQ

WAZIRI Mkuu wa Iraq, Adel Abdul Mahdi anatarajiwa kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu, baada ya zaidi ya watu 40 kuuawa ndani ya siku moja tangu kuanza kwa maandamano ya kuikosoa Serikali, ofisi yake imeeleza.

Kiongozi wa juu wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia amekemea matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji na kutaka kuwepo kwa Serikali mpya.

Karibu watu 400 wameuawa wakati wa maandamano tangu mwanzoni mwa Oktoba, na takribani watu 15 waliuawa siku ya Ijumaa.

Raia wa Iraq wanataka kazi na kukomesha vitendo vya rushwa pia huduma nzuri kwa Umma.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alisema “amesikitishwa sana na ripoti kuhusu muendelezo wa matumizi ya silaha dhidi ya waandamanaji” na kutaka matukio hayo yakome.

Katika taarifa yake jana, ilisema atawasilisha waraka wake wa kujiuzulu bungeni ili wabunge wachague Serikali mpya.

“Nikichukua hatua baada ya wito huu, na ili kuhakikisha linafanyika kwa haraka, nitawasilisha bungeni waraka wa kukubali kujiuzulu nafasi yangu ya uongozi wa serikali ya sasa,” taarifa yake iliyotiwa saini na Abdul Mahdi ilieleza.

Taarifa haikusema atajiuzulu lini. Jana, Bunge lilikaa kwa dharura kujadili hali ilivyo nchini Iraq.

Ijumaa Ayatollah Sistani alisema Serikali inaonekana “imeshindwa kushughulikia matukio yaliyojitokeza kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita”.

Kiongozi huyo alisema mashambulizi dhidi ya waandamanaji “ni marufuku” na pia aliwataka waandamanaji kuepuka vurugu na “kuacha vitendo vya uhalifu”.

Mahdi alishakuwa na nia ya kujiuzulu kabla lakini kuingilia kati kwa kiongozi wa kidini, kunafanya mambo kuwa tofauti hivi sasa.

Kinachotokea Iraq ni sehemu ya wimbi la maandamano katika eneo la ukanda, miongoni mwa maandamano hayo yanasababishwa na hasira ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 30 ambao wamechoshwa na hali ya ukosefu wa ajira, huduma mbovu za umma na vitendo ya rushwa vinavyodaiwa kufanywa na viongozi nchini humo.

Mahdi alishika nafasi hiyo kipindi cha mwaka mmoja uliopita, akiahidi mabadiliko, ahadi ambayo haijatekelezwa. Vijana wa Iraq waliingia kwenye mitaa ya Baghdad kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa mwezi Oktoba.

Baada ya maandamano ya kwanza yaliyodumu kwa siku sita na kugharimu maisha ya watu 149 Mahdi aliahidi kufanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri na kupunguza mishahara ya maofisa wa juu, na alitangaza pia kushughulikia suala la ukosefu wa ajira.

Lakini waandamanaji wanasema kuwa matakwa yao hayajatimizwa na kurejea tena mitaani mwishoni mwa mwezi Oktoba. Maandamano yalifanyika nchi nzima baada ya maofisa wa usalama kutumia nguvu kuwadhibiti waandamanaji.

Mkurugenzi wa utafiti kutoka Amnesty International eneo la Mashariki ya Kati, Lynn Maalouf, alivishutumu vikosi vya usalama kutumia nguvu siku ya Alhamisi dhidi ya waandamanaji.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles