31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU IRAK AONGOZA UCHAGUZI

BAGHDAD, IRAK


WAZIRI Mkuu wa Irak, Haieder al Abadi anaongoza uchaguzi wa Bunge uliofanyika juzi, kwa mujibu wa matokeo ya awali jana.

Uchaguzi huo unakuja tangu nchi hiyo itangaze ushindi dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS).

Kiongozi wa kidini wa madhehebu ya Shia, Muqtada al Sadr aliyegombea kwa niaba ya muungano wa vyama vinavyoiunga mkono Iran anashikilia nafasi ya pili katika matokeo hayo.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa leo  na Tume Huru ya Uchaguzi ya Irak, ambayo imeeleza kuwa idadi iliyojitokeza kupiga kura ni ndogo.

Asilimia 45 ya wapiga kura ndio waliojitokeza kushiriki kwenye zoezi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles