25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI MKUU AHUKUMIWA MIAKA 10 GEREZANI

 

ISLAMABAD, PAKISTAN

MAHAKAMA  imemhukumu aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif kifungo cha miaka 10 gerezani kwa makosa ufisadi unaohusu majengo manne ya kifahari jijini London nchini Uingereza.

Nawaz Sharif,ambaye kwa sasa yuko London alihukumiwa akiwa hayuko mahakamani, na mwenyewe alisema kuwa hukumu hiyo ina mlengo wa kisiasa.

Jaji Mohammad Bashir amemtaka Sharif kutumikia kifungo cha miaka 10 kwa kosa la kumiliki mali yenye gharama kubwa kuliko kipato chake na mwaka mmoja kwa kutotoa ushirikiano na mamlaka inayopambana na vitendo vya rushwa, NAB.

Binti yake, Maryam Nawazi Sharif amehukumiwa kifungo cha miaka saba kwa kushirikiana na baba yake kwenye uhalifu huo na mwaka mmoja kwa kutotoa ushirikiano kwa mamlaka za kiuchunguzi huku mkwewe Nawaz akihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kutotoa ushirikiano.

Sharif na Maryam wametozwa faini ya pauni milioni 8 na pauni milioni mbili. Kwa sasa wote wako jijini London ambapo mke wa Sharif, Kulsoom Nawaz anapata matibabu kutokana na maradhi ya saratani.

Kashfa ya Panama Papers iliyovuja mwaka 2015 ilitoa taarifa kuwa watoto kadhaa wa Sharif walikuwa na mahusiano na makampuni yaliyo nje, ambayo yalidaiwa kupitisha fedha kwa ajili ya kununua mali nje ikiwemo majengo ya anasa jijini London.

Familia yake,  inasisitiza kuwa wanamiliki mali hizo kihalali. Katika sehemu ya hukumu, Mahakama imetaka mali hizo zitaifishwe kwa serikali.

Waandishi wa habari nchini Pakistani walikita kambi nje ya makazi ya Avenfield, ambako familia ilikuwa ikitazama kesi.

Hukumu imetolewa wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu wa Pakisani utakaofanyika  Julai 25  mwaka huu. Sharifu amepoteza uhalali wa kukiwakilisha chama chake cha PML-N.

Kaka yake Shahbaz Sharif hivi sasa anakiongoza chama cha PML-N, na anawania katika uchaguzi huo ujao. Shahbaz amemtetea kaka yake katika mkutano na waandishi wa habari akisema kuwa hukumu hiyo ina ushawishi wa kisiasa.

Mahakama ya juu ilimvua madaraka Nawaz Sharif Julai mwaka 2017 baada ya taarifa ya Panama papers.

Shariff alikuwa madarakani tangu mwezi Novemba mwaka 1990 mpaka julai mwaka 1993 na kuanzia Februari mwaka 1997 mpaka alipoangushwa mwezi Oktoba mwaka 1999.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles