33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu aagiza eneo la Kiomoni litathminiwe

           Bethsheba Wambura, Dar es Salaam



 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha kwenda katika Kata ya Kiomoni iliyopo mkoani Tanga kufanya tathmini ya ardhi ya wananchi ili kubaini thamani halisi ya maeneo hayo ili wafidiwe.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni Jumanne Oktoba 30, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya hiyo katika mtaa wa Kiomoni wilayani Tanga ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga.

Alisema atamuagiza mtahamini mkuu aende kubaini nani anadai nini na anamiliki nini ili atoe kibali cha ulipwaji na mwekezaji aweze kupewa kibali cha kulipa fidia wananchi hao.

Hatua ya Waziri Mkuu imekuja baada ya wananchi wa eneo hilo kumlalamikia kutoridhishwa na fidia ya maeneo yao yaliyochukuliwa na kampuni ya Neelkanth inayomiliki kiwanda hicho cha kuzalisha chokaa.

“Tunataka jambo hili liishe kabla ya mwishoni mwa mwaka huu kila kitu kiwe kimekamilika na hakuna mwananchi hata mmoja atakayepoteza haki yake ya msingi, ” alisema.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa uwekezaji huo ni muhimu kwa kuwa ni sehemu ambayo viwanda mbalimbali vya saruji nchini vinategemea kwa kupata malighafi.

Alisema wawekezaji katika sekta ya viwanda ni muhimu kwa sababu wanaunga mkono mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi kutoka chini hadi wa kati ifikapo 2025 kwa kupitia sekta ya viwanda, uwepo wa kiwanda hicho utawezesha kukuza uchumi Taifa na wananchi kwa  sababu  kitakapokamilika kitatoa ajira ya watu zaidi ya 2,000.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mkinga leo Jumatano, Oktoba 31, akutane na wananchi wa kijiji hicho na kusikiza kero mbalimbali zinazowakabili ili aweze kuzitatua.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles