27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI LUGOLA ATANGAZA MAKANISA,MISIKITI

 

Na ELIYA MBONEA-Arusha

MAKANISA na misikiti yenye  migogoro isiyoisha ya kugombania uongozi, zaka na sadaka kufutwa hivi karibuni.

Agizo la kufutwa kwa nyumba  za ibada,limetolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola alipokuwa akizundua tamasha la kuombea amani Taifa.

Tamasha hilo, lililoandaliwa na Taasisi ya  Amos ya jijini Dar es Salaam, alilizindua jana katika Kanisa la Free Pentecostal Tanzania (FPCT), Jerusalem City Church lililopo Leganga wilayani Arusha mkoani Arusha.

Akizungumza na waumini wa kanisa hilo, baada ya maombi kwa Taifa, Rais Dk.John Magufuli, Baraza la Mawaziri, Waziri Lugola alisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakikimbilia kwa viongozi wa kitaifa kuomba suluhu ya migogoro inayowakabili.

“Nataka niwaambie ukiulizia ati wanagombea nini hawa viongozi kwenye nyumba za ibada utaskia ati Sadaka na uongozi,” alisema Waziri Lugola na kuongeza:

“Na hawa viongozi wanagombea ili wazifikie sadaka hizo, sasa naomba niwaambie wizara yangu ndio inayosajili makanisa na msikiti nchi hakuna mahali popote panaoonyesha vigezo vya sadaka na uongozi.

“Mizozo na uchonganishi makanisani na misikitini, naomba niwaambie vinamkera Rais Dk.Magufuli hasa anapoisikia ikiendelea mara kwa mara.

“Kwakuwa ameniteua kuwa msaidizi wake kwenye eneo hili, natangaza kuanzia sasa hapa kanisani kanisa au msikiti wowote utakaokumbwa na migogoro na kushindwa kutatua nitaufuta mara moja.

“Nitafanya hivi ili tubakie na nyumba chache cha ibada, niwaombe hakikisheni mnakuwa makanisa na nyumba za ibada zinazodumisha amani na utulivu wa nchi, alisema Waziri Lugola.

Kwa upande wake, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Joe Gahu alisema, zipo baadhi ya nchi ambazo watu huvamia kijiji na kuchinja watu hovyo hatua ambayo kwa Tanzania jambo hilo ni vigumu kutokea kutoka na neema ya Mungu kwa viongozi.

“Tanzania hatutakubali, tupo pamoja na Serikali kuhakikisha amani ya nchi yetu inaendelea kudumishwa na kulindwa,” alisema Mch.Gahu.

Naye mwanaandaaji wa maombi hayo,yanayotarajiwa kufanywa nchi nzima, Amos Mulungu alisema, kilichowasukuma ni kuunga mkono juhudi za serikali za kufikia uchumi wa kati.

“Ili kufikia uchumi wa kati, nchi lazima iwe na amani, tumeamua kuzunguka nchi nzima ili kuhamasisha na kuombea amani itakayotupeleka kuwa taifa lenye uchumi wa kati,” alisema Mulungu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles