24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI: FIGO KUANZA KUPANDIKIZWA NCHINI

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, amesema Serikali imejipanga kuanza kutoa huduma za upandikizaji wa figo nchini.

Kauli hiyo aliitoa juzi mjini hapa wakati akifungua mkutano wa nne wa Chama cha Wataalamu wa Figo Tanzania.
Dk. Ndugulile alisema kwamba, Serikali imekuwa ikipeleka wastani ya wagonjwa 35 kwa mwaka nje ya nchi ikiwamo India kwa ajili ya kupandikiza figo.

“Wagonjwa ambao walishapandikizwa figo na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni takribani 204.

“Gharama za kupandikiza figo nje ya nchi ni wastani wa fedha za Kitanzania shilingi milioni 75,000 hadi 77,000 kwa mtu mmoja.

“Kwa hapa nchini, upandikizaji wa figo bajeti ya mgonjwa mmoja ni shilingi milioni 20.3.

“Hiyo inamaanisha kwamba, kwa bajeti ya kupeleka mgonjwa mmoja nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza figo ni kubwa kwa sababu hapa nchini wanaweza kuwapatiwa huduma hiyo wagonjwa watatu hadi wanne.

“Kwa maana hiyo, huduma hizo zikianza kutolewa nchini, zitaipunguzia mzigo Serikali na Watanzania na pia tutaweza kuwafikia wagonjwa wengi zaidi,” alisema Dk. Ndugulile.

Kwa upande wake, Daktari Bingwa kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dk. Alfred Jackson, alisema wao wapo katika maandalizi ya upandikizaji wa figo nchini.

“Sisi hatupo nyuma na maandalizi yetu yanaendelea vizuri ikiwezekana Machi mwakani, tutaanza kushirikiana na wadau wetu kutoka Japan kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles