24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WAZIRI ATUMIA BAISKELI KWENDA KUJIFUNGUA HOSPITALI

WELLINGTON, NEW ZEALAND                  |                      


WAZIRI wa Masuala ya Wanawake nchini hapa, Julie Center, ameendesha baiskeli hadi hospitali kujifungua mtoto wake wa kwanza.

Genter kutoka Chama cha Kijani, alisema alitumia baiskeli aliyoiendesha mwenyewe baada ya kukosekana nafasi ya kutosha ndani ya gari.

Alipiga picha na mumewe wakiwa katika safari hiyo ya kutumia baiskeli na kuiweka katika akaunti yake ya Instagram.

Juni mwaka huu, Mbunge Jacinda Ardern, alikuwa mwanasiasa wa pili kujifungulia akiwa kazini na wote yeye na Genter walikua wakihudhuria Clinic pamoja katika hospitali ya umma mjini Auckland.

Genter (38) anayejulikana kama shabiki mkubwa wa matumizi ya baiskeli, aliandika katika mtandao wake wa Instagram; “mtuombee baraka, mimi na mwenzangu tumepanda baiskeli kwa sababu hakukuwa na nafasi kwenye gari kutokana na kujaa wasindikizaji.”

Waziri huyo atakayechukua miezi mitatu ya likizo ya uzazi, ataungana na baadhi ya wanasiasa waliopata watoto wakati wanatumikia nafasi za kisiasa.

Mbunge wa kwanza kupata mtoto akitumikia Bunge la New Zealand, ilikuwa mwaka 1970, huku mwingine akinyonyesha kwa mara ya kwanza katika eneo la kazi mwaka 1983.

Nao Austalia walibadilisha kanuni mwaka 2016 kuruhusu watungasheria kuweka sheria ya kunyonyesha katika eneo maalumu ndani ya Bunge.

Katika miaka ya hivi karibuni, Sweden, Italia na Bunge la Ulaya wamegusa ulimwengu kwa kupiga kura bungeni wakiwa wamebeba watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles