23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri ataka Stars kupigana kufa au kupona Afcon

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, amewataka wachezaji wa timu ya Tanzania, Taifa Stars, kwenda kupigana kufa au kupona katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), itakayoanza Juni 21, mwaka huu, nchini Misri.

Juliana aliyasema hayo jana wakati akikabidhi Bendera ya Taifa timu hiyo k kwenye Hoteli ya Whitesands, Kunduchi, Dar es Salaam.

Kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kuondoka leo jioni kuelekea Misri ambako kitaweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na michuano hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Juliana aliwataka wachezaji wa timu hiyo kuonyesha nidhamu zaidi kwenye michuano hiyo.

Juliana alisema  Taifa Stars imevuka hatua moja ya kufuzu michuano hiyo,  hivyo wanatakiwa kuvuka na nyingine ya kwenda kushinda ili wafike mbali zaidi.

“Kwenye mashindano kama haya, kitu cha muhimu ni nidhamu, mshikamano na umoja, kwani bila hayo mambo hamtaweza kufanya vizuri, ukizingatia macho ya Watanzania yote yapo kwenu, tunawaomba mkatuwakilishe vyema.

“Sisi kama Serekali tutakuwa na nyie bega kwa bega katika kuhakikisha mnafanya vizuri michuano hiyo, kwani mmeona hata Mheshimiwa Rais John Magufuli alivyokuwa akiwasapoti,” alisema.

Pia kama Serikali imemaliza kila kitu kuhusu kukabidhiwa hati za viwanja walivyohaidiwa na Rais Magufuli, ila kulikuwa na ucheleweshwaji wa majina kutumwa wizarani na watakabidhiwa hivi karibuni.

Upande wake,  kocha mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Amunike, alisema wanaenda Misri kupambana na kufanya kazi kwa nguvu ili wafanye vizuri.

“Tunawashukuru Watanzania wote kwa kuonyesha ushirikiano mzuri  na sisi tutaenda kupambana ukizingatia tuna kikosi kizuri ambacho kinaweza kuleta matokeo mazuri,” alisema.

Upande wake, nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta, alisema wanaenda kupambana na kuleta kitu ambacho kitailetea sifa Tanzania.

 “Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tunashukuru kwa kuwa hapa, kwani hata mara ya mwisho tulivyokuwa tunaenda kucheza na Uganda ulikuja na tukafanya vizuri, naamini ujio wako huu utakuwa wa baraka,” alisema.

Katika michuano hiyo, Tanzania imepangwa Kundi C,  pamoja na Algeria, Senegal na majirani zao Kenya.

Tanzania itaanza kucheza na Senegal Juni 23, mwaka huu,  kabla ya kuivaa Kenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles