33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi watakiwa kuwa na hofu ya Mungu

JEREMIA ERNEST

Walezi na wazazi nchini watakiwa kuwa na hofu ya mungu ili kuimarisha na kuendesha familia zao kiuchamungu.

Akizungumza na waaandishi wa habari wakati baada ya kutambulishwa kuwa mmoja wa balozi wa jukwaa la naweza linalosisitiza kuwa na familia zinazojali misingi ya afya, Hilal shaweji maarufu sheikh kipoozeo amesema kuna wakati watoto wanakumbwa na mikasa mingi ya malezi kwenye makuzi yao kutokana na kutokuwepo hofu ya Mungu katika familia zao na kusababisha matatizo.

“Unakuta baba mlezi anamlawiti mtoto wake bila ya hofu kuwa si jambo zuri katika jamii hata kwa Mwenyezi Mungu hivyo ili malezi yakamilike lazima pawepo hofu ya mungu ndani yake,” amesema Sheikh Kipoozeo.

Amesema kuwa malezi ya vijana yamekuwa mabaya mno hasa ukizingatia wazazi wengi wanakua na wakati mgumu kuanzia kwenye familia yenyewe kuwa na mpangilio mbaya wa uzazi kila mwaka ana mtoto unakuta hawezi kuwaangalia makuzi ya wale watoto wengine kama mwanzo kutokana na kulea mtoto mwengine na unakuta anasahau wale wengine makuzi yao.

Sheik Kipoozeo anaungana na Masoud Kipanya, Zuwena Mhamed ‘Shilole’ na  Mwijaku katika kampeni hii ya Naweza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles