25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wazazi wapigwa marufuku kufanya biashara na watoto sokoni

Upendo Mosha – Moshi

Uongozi wa soko kuu la mitumba la Memorial, Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, umeahidi kushirikiana na jeshi la Polisi kupiga marufuku wafanyabiashara wa soko hilo kwenda sokoni hapo na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa soko hilo, Godfrey Shayo, leo Juni 24, wakati wa utafiti wa kuongeza uelewa, uwajibikaji wa huduma bora za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto (ECD),  zoezi linalo tekelezwa na muungano wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) kwa kushirikiana na taasisi ya CIC ya Ireland

“Ukija sokoni hapa majira ya saa 11 Alfajiri utaona wazazi na walezi wakiwa na watoto wachanga huu ni ukatili na unaathiri afya ya mtoto na malezi yake ya baadaye, tumeliona hili na tunaandaa mpango wa kutoa elimu kabla ya kuchukua hatua” amesema.

Kwa upande wake mwenyekiti wa masoko la Mbuyuni, Lameck Mziray na mwenyekiti mtaa wa soko la Pasua, Rahibu Juma walikiri kuwapo kwa changamoto inayoathiri afya za watoto hao lakini wameahidi kuandaa mpango wa ushirikishwaji na wafanyabiashara ili kujadili suala hilo.

Naye Daktari bingwa mwandamizi wa afya ya jamii, Uzazi  na magonjwa ya akina mama, Dk  Moke Magoma amesema malezi hayo yasipothibitiwa yatachangia kwa asilimia kubwa kujenga taifa la kizazi kisicho na mwelekeo na chenye urahisi wa kujihusisha na matukio ya uhalifu.

Aidha kabla ya kufanyika kwa zoezi hilo, uongozi huo utatoa elimu kwa wazazi na walezi wenye watoto  kuanzia miaka sifuri hadi mitano ambao wanaonekana sokoni hapo kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa moja usiku wakiwa na wazazi wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles