24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘Wazazi acheni kuozesha watoto wenye umri mdogo’

Elizabeth Kilindi-Njombe

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Mkongea Ali, amewataka wazazi na walezi wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe kuacha tabia ya kuwaozesha watoto wa kike wakiwa na umri mdogo.

Pia amesema anachukizwa na tabia ya wanawake kuchukua vyandarua kuwapa waume zao na kwenda kuvulia samaki.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizindua bweni la wasichana Shule ya Sekondari Wanging’ombe pamoja na kuzindua majengo katika kituo cha afya.

Pia alipongeza juhudi za Rais Dk. John Magufuli kwa kutoa fedha ili kuhakikisha anapambana na adui ujinga pamoja na kusogeza huduma za afya kwa wananchi.

“Kuna vyandarua ambavyo vinatolewa bure bila ya malipo ya aina yoyote, tutumie kama ambavyo tumeelekezwa, ila cha kusikitisha kuna maeneo ambayo tumepita vyandarua wanapewa kina mama, wanawapa waume zao kuvulia samaki, hili si sahihi. Pia tunaona baadhi ya watu wanavitumia katika bustani ili mifugo isiweze kuingia.

“Tuache tabia ya kuwaozesha watoto wakiwa wadogo ni jambo la ajabu sana mtoto wa kike ni sawa kama watoto wengine na ana haki ya kupata elimu kama ilivyo kwa watoto wengine,” alisema Ali.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa bweni la wasichana kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge,  Mkuu wa Shule ya Sekondari Wanging’ombe, Optatus Mng’ong’o, alisema ujenzi huo umejengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wote wa kike wanaishi katika mazingira ya shule.

“Bweni hili limejengwa ili kuwaondolea usumbufu wanafunzi kupanga mitaani, ambako kuna hatari kubwa ya kurubuniwa na wanaume wasio na maadili mema na kisha kusababisha kupata mimba zisizotarajiwa na hatimaye kukatisha masomo yao,” alisema Mng’ong’o.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles