25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wayne Rooney apanga kuwa kocha

Wayne Rooney
Wayne Rooney

MANCHESTER, ENGLAND

NYOTA wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England, Wayne Rooney, ameweka wazi kuwa atakuja kuwa kocha mara baada ya kustaafu soka 2019.

Maneno hayo yamekuja mara baada ya nahodha wa zamani wa timu hiyo, Alan Shearer, kumtaka mchezaji huyo astaafu kuitumikia timu ya taifa na nguvu zake azipeleke katika klabu yake ya Manchester United.

Rooney amesema kuwa kwa sasa ana mkataba na klabu yake ya Manchester United hadi 2019, hivyo akimaliza mkataba huo atastaafu na kujitupa kwenye mambo ya ukocha.

Hata hivyo, mchezaji huyo amesema kuwa anatarajia kuachana na timu ya taifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018.

“Bado kwa sasa nina majukumu ya kuitumikia timu ya taifa, nimepanga kustaafu baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia 2018, natarajia kujitoa kwa ajili ya taifa langu katika michuano hiyo mikubwa na baada ya hapo nguvu zangu nitazielekeza katika klabu yangu kwa msimu mmoja mbele.

“Kwa upande wa Manchester United bado nina nafasi ya kuitumikia klabu hiyo baada ya kocha mpya Jose Mourinho kunipa majukumu ya namba 10 nikiwa uwanjani.

“Nitakuja kuachana na klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wangu 2019, baada ya hapo nitaendelea na majukumu mengine kwenye soka.

“Siwezi kustaafu halafu nikaachana kabisa na mambo ya soka, ninaamini nitakuwa kama wachezaji wengine ambao wanakimbilia kwenye masuala ya ukocha kwa kuwa ninaamini naweza kuwa kocha.

“Muda mrefu sasa nimekuwa nikipata mafunzo ya ukocha lakini sina uzoefu, ila ninaamini baada ya kumaliza maisha yangu ya kucheza soka nitakuwa na uwezo mkubwa bila ya kujali uzoefu,” alisema Rooney.

Nahodha huyo tayari amejiunga na timu hiyo ya taifa chini ya kocha wake, Sam Allardyce, kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Slovakia wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018, mchezo huo utapigwa Jumapili mwishoni mwa wiki hii.

Rooney alishindwa kuonesha uwezo mkubwa katika michuano ya Kombe la Euro 2016 nchini Ufaransa, huku timu yake ya England ambayo ilionekana kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa wakiyaaga mashindano hayo mapema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles