27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

WAWEKA MIKAKATI KUKABILI UKEKETAJI ILALA

Ofisa Programu Utetezi na Ushawishi kutoka TGNP Mtandao, Deogratius Temba

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


VIONGOZI wa Serikali za Mitaa na Jeshi la Polisi wameshauriwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji vinakomeshwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza juzi wakati wa mjadala wa Bunge la Jamii uliohusisha viongozi wa mitaa yote ya Kata ya Kitunda, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, walimu wa shule za msingi na sekondari, Jeshi la Polisi na wadau wa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, Ofisa Programu Utetezi na Ushawishi kutoka TGNP Mtandao, Deogratius Temba, alisema vita dhidi ya ukeketaji wa wasichana ndani ya Manispaa ya Ilala itafanikiwa endapo wadau wote watashirikiana.

Mjadala huo ni sehemu ya mradi wa kupambana na mila potofu zinazosababisha kuendelea kwa vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto unaofadhiliwa na Foundation for Civil Society (FCS).

Katika mjadala huo, wadau kwa pamoja walikubaliana kuunda kamati za kutokomeza ukatili wa kijinsia ngazi za mitaa kama sehemu ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa miaka mitano wa kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto (NPA) unaotekelezwa kuanzia mwaka 2016/17 hadi 2021/22.

“Tumekubaliana hapa kuunda kamati za kutokomeza ukatili wa kijinsia, taarifa zipo kwetu sisi wananchi, unapomwona jirani yako anapanga sherehe za kumkeketa msichana wa shule, toa taarifa kwa kamati au kwa mtendaji wa kata ili hatua zichukuliwe,” alisema Temba.

Mtendaji wa Kata ya Kitunda, Hamza Juma, alisema vita dhidi ya ukatili wa kijinsia inawezekana endapo watendaji wa mitaa, wenyeviti na maofisa maendeleo ya jamii wa kata watawajibika ipasavyo na kuhakikisha taarifa za ukatili zinawafikia polisi kwa wakati ili hatua zichukuliwe.

“Kuna kazi nzuri inafanywa na Jeshi la Polisi, lakini tunahitaji kuwapa ushirikiano wa kutosha ili hata wale wanaokeketa wasichana wa shule tutoe taarifa zao mapema na hatua zichukuliwe,” alisema Juma.

Kwa mujibu wa jamii zinazofanya ukeketaji, mwaka huu ni mwaka wa ukeketaji na kwa Dar es Salaam, kata za Kivule, Kitunda, Kipunguni, Mzinga, Msongola, Pugu na Chanika zinatajwa kuwa na idadi kubwa ya watoto walio hatarini kukeketwa ifikapo Novemba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles