30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wauguzi kukagua watoto waliokeketwa

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangalla.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangalla.

NA GABRIEL MUSHI, DODOMA

SERIKALI inatarajia kuzindua  mpango kuawezesha wauguzi  kufahamu jinsi  ya kuwakagua watoto wa kike hususani wachanga   wanapofikishwa  kliniki ili kubaini waliofanywa ukeketaji.

Hatua hiyo pia itawezesha  wazazi wao kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kauli hiyo ilitolewa  bungeni  Dodoma jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangalla wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Fatma Hassa Toufiq (CCM).

Mbunge huyo  alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kufuatilia wa kuwanusuru watoto wachanga wanaokeketwa na wazazi wao kukwepa mkono wa sheria.

Naibu waziri alisema serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inazindua Mpango Kazi wa Taifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto 2017-2022  wenye lengo la kutokomeza masuala ya ukatili na mila zinazosababisha ukeketaji wa watoto wa kike.

Dk.  Kigwangalla alisema serikali inaendelea kuelimisha vikundi mbalimbali kwa kupitia mangariba kwa kuanzisha madawati zaidi ya 417 ya jinsia na watoto katika vituo vya polisi.

Vilevile itaanzisha mtandao wa huduma ya mawasiliano ya kuwasaidia watoto   na   timu za ulinzi wa mtoto katika kila halmashauri mbalimbali  kukabili tatizo la ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Alisema mpango huo unatarajiwa kuzinduliwa mwezi huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles