31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WATUMISHI MANISPAA MOROGORO MBARONI KWA RUSHWA

Na LILIAN JUSTICE-MOROGORO


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Morogoro (Takukuru), imewapandisha kizimbani watuhumiwa wawili wa Serikali kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi.

Watumishi hao wameshtakiwa kwa kughushi nyaraka za kubadili matumizi ya fedha.

Walifikishwa mahakamani jana, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Agripina Kamaze ambapo mwendesha mashtaka wa Takukuru, Cleonce Cleophace alidai mahakamani hapo kuwa, Herman Msuha ambaye ni Ofisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro, anadaiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Alidai zaidi kuwa mshtakiwa, kati ya Juni 1 hadi Desemba 31 mwaka 2015, alishindwa kuondoa jina la mtumishi wa manispaa, marehemu Julius Maliyanga kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi kwa kipindi tajwa.

Mwendesha mashtaka huyo alidai mshtakiwa amefunguliwa kesi ya jinai namba120/2018 kwa kutumia mamlaka yake vibaya akiwa Ofisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro, kitendo ambacho ni kosa chini ya kifungu cha sheria namba 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, namba 11 ya mwaka 2017.

Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kudai mahakamani kuwa mshtakiwa anadaiwa kuisababishia Serikali hasara ya jumla ya Sh milioni 2.5, jambo ambalo ni kosa chini ya sheria ya uhujumu uchumi.

Mshtakiwa huyo alikana makosa yote na yupo nje kwa dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena Juni 19, mwaka huu.

Katika tukio jingine, mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tubuyu, Henry Mbawala na mwenyekiti wake wa bodi ya shule hiyo, Robert Leole wanatuhumiwa kwa makosa ya kughushi.

Mbele ya Hakimu Kamaze, mwendesha mashata huyo alidai kuwa washtakiwa hao wanashatakiwa kwa kughushi muhtasari wa kikao cha bodi ya shule cha Januari 8, 2018 na kuonesha kuwa Kampuni ya Tweyambe Agricultural and General Enteprises Co. Ltd, imeshinda zabuni ya ukarabati wa vyumba vya madarasa vya shule hiyo, jambo ambalo si kweli.

Washtakiwa hao walikana kosa hilo na wapo nje kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena, Juni 19, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles