31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WATUMIAJI DAWA ZA KULEVYA MBEYA WAONGEZEKA

Na IBRAHIM YASSIN- MBEYA

IDADI ya watumiaji wa dawa za kulevya Mkoa wa Mbeya, imeendelea kuongezeka.

Idadi hiyo imeongezeka kutoka   asilimia 20 hadi kufikia asilimia 25 kwa miaka  tofauti.

Takwimu hizo zimetolewa jana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya ya Akili, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dk. Paul Lawala, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

Akitoa takwimu hizo, Dk. Lawala alisema kama hali hiyo isipodhibitiwa inaweza kuwa mbaya zaidi.

“Hali inazidi kuwa mbaya zaidi na zinahitajika nguvu za ziada ili kukabiliana na hali hiyo vinginevyo waathirika watazidi kuongezeka,” alisema Dk. Lawala.

Naye Makalla alikemea matumizi ya dawa hizo na kusema yeyote atakayekamatwa akijihusisha na biashara ya dawa hizo, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Vyombo vya ulinzi na usalama lazima muwe macho kudhibiti matumizi ya dawa hizo na yeyote mtakayemkamata mfikisheni katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Makalla.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, alisema idadi kubwa ya waathirika wa dawa hizo ni vijana.

“Kwa hiyo tumeanza mipango kabambe ya kukabiliana na matumizi ya dawa hizo na atakayekamatwa atafikishwa katika vyombo vya sheria,” alisema Kamanda Kidavashari.

“Kwa hiyo nawaomba wananchi tushirikiane katika vita hii kwa sababu bila ushirikiano hatutaweza kufanikiwa kwa asilimia mia moja,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles