25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Watu watano wafariki dunia kwa ajali

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa.

Na Upendo Mosha, Same

WATU watano wamefariki dunia papohapo na wengine wanne kujeruhiwa  vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari la mizigo wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa, alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 10: 45 alfajiri  katika eneo la Alikacheje Sekondari, Kijiji cha Makanya wilayani Same.

Alisema gari  ya Toyota Noah nambari   T933 DFY   iliyokuwa  imebeba magazeti ya MTANZANIA yanayochapishwa na Kampuni ya New Habari (2006) Limited, ilikuwa  ikitokea  Dar es Salaam kwenda  mkoani Arusha  liligongana uso kwa uso na gari ya mizigo  nambari T.532 DFQ Scania semi trailer  na kusababisha vifo hivyo   na majeruhi hao.

“Gari hilo la mizigo lililokuwa likitoka Babati kwenda mkoani Tanga na kuendeshwa na  dereva aliyefahamika kwa jina la Riziki Mandoo mkazi wa Karatu mkoani Arusha, liligongana na gari hiyo   ya Noah na kusababisha vifo vya watu watano papohapo ambao  wote walikuwa ni wanaume  akiwamo dereva wa Noah aliyefahamika,   Kiwanga Dominick (37) mkazi wa Kahe wilayani Moshi pamoja na majeruhi wane,” alisema.

Alisema   miili miwili ya marehemu ndiyo iliyotambulika ikiwamo ya dereva wa gari hilo pamoja na mtu mmoja,    Inocent Massawe (25), mkulima na mkazi wa Kibosho huku marehemu wengine watatu wakiwa bado hawajaweza kutambulika.

Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Juma Kobasi (36) Simon Kaaya, Lita Ulutu (46) na Bakari Mndeme (31) na  majeruhi watatu kati yao wamepelekwa kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa  KCMC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles