29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 34 hoi kwa kipindupindu Dar

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

UGONJWA wa kipindupindu umezidi kushika kasi mkoani Dar es Salaam, baada ya idadi ya wagonjwa kuongezeka kutoka 27 hadi 34.

Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaama jana, Mratibu wa Huduma za Dharura, Mkoa wa Dar es Salaam, Victoria Bura alisema kumekuwapo na ongezeko la ugonjwa huo katika Wilaya ya Kinondoni.

Alitaja maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo kuwa ni Kijitonyama, Makumbusho, Saranga, Manzese, Tandale, Kimara na Mwananyamala.

Kwa mujibu wa Bura, wagonjwa watatu kati ya hao wamefariki dunia na wengine wane wameruhusiwa baada ya afya zao kuimarika.

“Kumekuwapo na ongezeko la wagonjwa wapya saba, hali hii inaonyesha tatizo lipo katika maeneo hayo niliyotaja.

“Takwimu zetu, zinaonesha hatuja pokea taarifa zozote kutoka wilaya za Ilala na Temeke, nawaomba  wakazi wa maeno mengine kuchukua hadhari kwa kuzingatia kanuni za usafi na kuepuka mikusanyiko ya watu isiyo ya lazima,”alisema.

Kutokana na hali hiyo, Bura aliwataka wananchi kufanya usafi katika maeneo  yao na hasa majumbani na wafanyabiashara  kama vile wauza matunda na mama lishe.

“Ili kufanikiwa kudhibiti ugonjwa huu, tunaziomba serikali za mitaa zisimamia jambo nyumba kwa nyumba, maana tunaamini wao ndiyo wako karibu zaidi na wananchi,”alisema Bura.

Kuhusu mgonjwa aliyefariki, alisema alifikishwa hospitalini akiwa anatapika na kuharisha dalili ambayo iliyoonesha kuwa amepatwa na ugonjwa huo.

Alisema familia yake nayo ilikuwa imepatwa na dalili ya  ya ugonjwa huo.

“Jumamosi  saa 2:00 asubuhi Hospitali ya Mwananyamala ilipokea mgongwa mwanamume mwenye umri wa miaka 50, akiwa amefariki dunia  kutokana na kuharisha na kutapika akitokea mtaa wa Ally Maua, Kijitonyama.

“Baada ya kufuatilia kwa kina,tulichukua hatua haraka kwa kutoa huduma kwa familia na kunyunyuzia dawa ya kuua vijidudu kwenye maji,”alisema.

Naye Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam, Judithi Kahama  alisema tayari kambi ya madaktari imewekwa  katika hospitali za Sinza na Mwananyala ili kutoa huduma zinazohitajika kwa wagonjwa.

Alisema kambi nyingine, zimewekwa katika Hospitali ya Mburahati, Buguruni na Temeke, huku zote zikiwa  na dawa za kutosha za kukabiliana na ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles