27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 32 wajiteketeza kwa moto kuweka rekodi ya Dunia

JOSEPH HIZA NA MITANDAO

WATU wenye kudhamiria kitu iwe chenye manufaa fulani kwa maisha yao, au ambacho kitaandika historia isiyofutikia huwa hawakati tamaa katika kufikia lengo walilojiwekea.

Hawa ni watu, ambao hawawezi kuwa na amani bila kufanikiwa malengo na ndoto zao.

Huwa hawajali ugumu au changamoto yoyote iliyopo mbeleni, wala kukata tamaa katika harakati za kufikia lengo lao.

Huweza kurudia njia moja au mbalimbali ama kufanya majaribio ya kufanikisha dhamira hizo.

Kwa sababu hiyo, huwa wana sababu nzito ya kutekeleza hiyo dhamira bila kujali iwapo kulifikia lengo hilo kunahitaji kuhatarisha kwanza maisha yao.

Kwao ni bora kuhatarisha maisha kuliko kukaa bila kujaribu vinginevyo ili wasije ishi maisha ya kujutia kutotimia kwa hiyo dhamira.

Watu hawa wanaweza kuwa na dhamira tofauti tofauti; wanaweza kuwa wenye malengo ya kibiashara, siasa, utajiri na hata kutaka tu kuweka rekodi au kumbukumbu ama tuseme historia na heshima.

Kundi la watu 32 nchini Afrika Kusini lililojiteketeza kwa moto katikati ya mwaka jana, katika tukio ambalo ndilo kusudio ya makala haya, ni moja ya watu wenye dhamira hizi.

Lililenga kuvunja na kuweka tu rekodi ya dunia, yaani kuingia katika vitabu vya kumbukumbu zitakazoishi kwa miaka mingi ijayo.

Unaweza kusema ni watu wenye wazimu, watu hawa waliojaa ujasiri wa kujiteketeza kwa moto kwa malengo ya kuingia katika rekodi mpya ya dunia kwa kuungua mwili mzima.

Bila kujali tukio hilo linaloweza kuonekana kutokuwa la maana au la kijinga, kuangalia watu wakiteketea vikali kwa moto na kisha mwishoni mwa tukio wakiruka ruka kushangilia ‘ushindi.’ Hakuna shaka ni sehemu ya utumbuizaji au kuburudisha watu.

Wataalamu wa mazingaombwe 32 walikusanyika mjini Cape Town, Afrika Kusini na taratibu kuanza kujiteketeza moto huku wakitembea kuufuata mstari wanaotakiwa kuishia. Ni kitu ambacho waliripotiwa kufanikiwa na kuvunja rekodi ya kundi kubwa zaidi la watu kujiteketeza pamoja moto mwili mzima.

Dhamira yao ikatimia kwa kufanikiwa kuingia katika Kitabu cha rekodi za dunia yaani Guinness Book of World Records.

Kanuni ya rekodi hii ya kutisha inasema kwamba wataalamu hao wa mazingaombwe wanapaswa kustahimili moto kwa sekunde 30. Waandaaji wa tukio hilo walilieleza kama la kuburudisha.

Washiriki hao 32 walitembea pamoja kuelekea mstari wa mwisho na mara walipomaliza walianguka sakafuni ili kusaidiwa kuzimwa moto uliokuwa ukiwaka kwa hasira miilini mwao.

Tukio hilo lililofanyika katika viwanja vya Grand Parade na kuandaliwa na Kevin Bitters, Grant Powell na Veron Willemse lilikuwa maalumu pia kwa kupromoti vipaji vya wasanii.

Lengo lilikuwa ni kupata kundi la watu wenye ujasiri wa kidunia na ujuzi wa aina yake kwa ajili ya kitu cha kufurahisha na kuburudisha.

Hata hivyo, licha ya hatari waandaaji waliratibu vyema tukio hilo kwa kuwa makini kuhakikisha usalama na afya ya washiriki hao wakati na baada ya tukio la kuteketea kwa moto.

Awali kabla ya rekodi hiyo ya watu wengi zaidi kuteketea moto kuvunjwa nchini Afrika Kusini, rekodi kama hiyo ilikuwa ikishikiliwa na wakazi wa mjini Cleveland, Ohio nchini Marekani.

Iliwekwa Oktoba 19, 2013 na watu 21, ambapo licha ya kufanikiwa kuingia katika kitabu cha Guinness Book of World Record, tukio hilo lilikuwa la kuchangisha fedha za taasisi moja ya hisani. Tukio hili la kuteketea kwa moto lilidumu kwa sekunde 32.

Na kabla ya rekodi hiyo, katika mji huo pia mwaka 2009, rekodi ya watu 17 iliwekwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles