27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto weusi, wavulana wanaongoza kwa kuchapwa viboko shuleni

mwanafunzi-akichapwaWAKATI tukio la walimu kutoa kipigo kwa mwanafunzi wa Sekondari ya Mbeya likishamiri kila kona katika vyombo vya habari na mitandao, taarifa zinaeleza kwamba nchini Marekani majimbo 19 tu ndio bado yamehalalisha adhabu ya viboko huku majimbo 31 yakiwa yamefuta adhabu hiyo kwa shule za umma.

Utafiti mpya uliofanywa na Elizabeth T. Gershoff  wa Chuo Kikuu cha Texas na Sarah A. Font  wa Chuo Kikuu cha Penn,  umeonyesha kwamba watoto weusi, wavulana na watoto wenye ulemavu ndio wanaoongoza kwa kuchapwa mara nyingi kuliko wenzao.

Adhabu hiyo ambayo hutolewa kwa kuchapwa na ubao au fimbo imekuwa ikitumiwa kwenye makosa makubwa kama vile mwanafunzi kuchoma moto shule, matumizi ya simu na kutofanya kazi za darasani wanazopewa na walimu.

Inakadiriwa kwamba mwaka 2003 wanafunzi 270,000 walichapwa viboko ambapo wanafunzi 10,000 hadi 20,000 waliumizwa kiasi cha kutafuta matibabu.

Majeraha waliyopata ni pamoja na ya michubuko, kuvunjika mifupa, kuteguka misuli na damu kuvimbia mwilini.

Mwaka 1977 Mahakama Kuu nchini humo ilitoa uamuzi kuwa adhabu ya viboko ipo kikatiba wakati huo ni majimbo mawili tu yalikuwa hayana adhabu hiyo kwa shule za umma.

Ripoti ya utafiti huo inaeleza kwamba hakuna ongezeko lolote la uhalifu wa vijana katika majimbo yaliyofuta adhabu hiyo.

Ripoti inaendela kueleza kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kutafuta njia mbadala za kufundisha nidhamu shuleni bila kusababisha maumivu ya mwili na kufanikiwa kuondoa kabisa uhalifu wa vijana.

Mwandishi wa ripoti hiyo anadokeza kuwa pamoja na kwamba katika majimbo mengi ya Marekani ni kosa kubwa kumpiga mnyama hadi kumuumiza, bado baadhi ya majimbo ambayo yanaruhusu viboko shuleni  hayatambui kosa la kumpiga mtoto hadi kumuumiza katika sheria zao.

Hiyo inaamaanisha kwamba katika baadhi ya majimbo mzazi atashtakiwa kwa kumpiga na kumuumiza mtoto lakini mwalimu hawezi kushatakiwa kwa kosa hilo.

Utafiti huo unaonyesha kutofautiana kwa matokeo kutokana na rangi na jinsi.

Mfano kwa majimbo ya Mississippi na Alabama asilimia 51 ya watoto weusi wanachapwa kuliko Wazungu na katika majimbo manane wavulana wanachapwa mara tano zaidi ya wasichana.

Imeandaliwa na Jonas Mushi kwa msaada wa mitandao

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles