23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WATOTO WA KIFALME KUFUNGUILIWA MASHITAKA SAUDIA

RIYADHI, SAUDI ARABIA


OFISI ya Mwendesha Mashitaka Mkuu nchini hapa imeanza kuchunguza tuhuma za rushwa zinazowakabili watoto wa ukoo wa kifalme, maafisa wa ngazi za juu na matajiri wa nchi hiyo waliokamatwa mwaka jana.

Makumi ya watu walikamatwa na kuzuiliwa katika Hoteli ya kifahari ya Riz-Carlton kwa amri ya Mwanamfalme Mohammed bin Salman, Novemba mwaka jana na kuhojiwa kuhusika na rushwa. Wengi wao, akiwemo tajiri mwekezaji mkubwa, Mwanamfalme Alwaleed bin Talal waliachiwa huru baada ya kuridhia kurejesha fedha hizo.

Wengine 56 ambao hawakufikia makubaliano hayo wanaendelea kushikiliwa rumande na wanaweza kufunguliwa mashitaka.

Naibu Mwanasheria Mkuu Saud Al Hamad anayeshughulikia utafiti ameliambia gazeti la Al Sharq Al Awsat yeyote atakayetuhumiwa ubadhilifu au ugaidi atafikishwa mahakamani.

Hakutoa maelezo zaidi kuhusu watuhumiwa hao. Kampeni ya kupambana na rushwa ni miongoni mwa juhudi za mwanamfalme Mohammed Bin Salman za kuifanyia mageuzi nchi hiyo ya kifalme ili isitegemee pekee utajiri wa mafuta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles