24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

WATOTO PIA WANAPASWA KUFANYA MAZOEZI


Dk. Fredirick L Mashili MD, PHP

Tunaendelea na mfululizo wa makala zetu tulizojifunza huko nyuma, ambapo tayari tumeshajikumbusha mambo 16 tuliyojifunza huko nyuma. Endelea… 

Kufanya mazoezi kwa kiwango chochote ni bora kuliko kutokufanya kabisa

Japo tumejifunza kwamba kuna kiwango cha mazoezi kinachoshauriwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), tufahamu pia kwamba kufanya mazoezi kwa kiwango chochote ni bora kuliko kutokufanya kabisa. Hii inamaanisha kwamba hata kama hutimizi kiwango kilichoshauriwa, unapata faida za kiafya kuliko yule asiyefanya kabisa 

Mazoezi yanapaswa kuwa tabia

Tunaposema mazoezi ni kinga na tiba, tukumbuke kwamba tofauti na ilivyo kwa dawa mfano za malaria, unapofanya mazoezi kama sehemu ya kinga au tiba, unatakiwa kufanya hivyo siku zote.

Kwa maana hiyo ni muhimu kuyafanya mazoezi kuwa tabia. Wengi wetu huacha mara tu tunapofikia malengo tuliyokuwa tumejiwekea na kujisahau kwamba kufanya mazoezi ni zoezi endelevu. 

Kufanya mazoezi husaidia kuzuia na kudhibiti msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo au stress ni tatizo linalowakabili watu wengi. Tunafahamu kwamba msongo wa mawazo ukizidi huweza kuathiri utendaji kazi na maisha kwa ujumla. Kufanya mazoezi mara kwa mara na kushiriki katika michezo husaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia na kudhibiti tatizo hili. 

Kufanya mazoezi husaidia kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa sonona

Sonona ni hali ya kujisikia huzuni iliyopindukia. Mara nyingine humfanya mtu kutamani kujidhuru na hata kukatisha maisha yake. Kufanya mazoezi mara kwa mara husaidia kuongeza vichocheo ambavyo ni muhimu katika kuzuia na kuidhibiti hali hii. Lakini pia kushiriki katika mazoezi ya vikundi hutoa fursa ya kukutana na watu mbalimbali jambo ambalo ni muhimu katika kuzuia na kudhibiti tatizo la sonona. 

Unaweza kupata mwonekano au umbo ulipendalo kwa kufanya mazoezi

Pamoja na faida lukuki kwa afya zetu, tumejifunza pia kwamba upo uwezekano wa kupata umbo au mwonekano tuupendao kwa kufanya mazoezi. Kwa kufanya aina zote tatu za mazoezi tunaweza kupata umbo na mwonekano tunaoupenda. 

Watoto pia wanatakiwa kufanya mazoezi

Kama ilivyo kwa watu wazima, watoto pia wanashauriwa kufanya mazoezi. Kutokufanya mazoezi huwafanya wawe wazembe, wanene kupindukia na wenye uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa sugu kama kisukari. Watoto wanashauriwa kushiriki katika michezo shuleni na nyumbani, kutembea au kuendesha baiskeli pamoja na kufanya mazoezi maalumu. Viko viwango vya mazoezi vinavyoshauriwa ili kudumisha afya yao. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles