Imechapishwa: Fri, Oct 27th, 2017

WATOTO PACHA WALIOUNGANA VICHWA WATENGANISHWA INDIA

Jopo la Madaktari 30 wa upasuaiji katika mji mkuu wa India Delhi wamefanikiwa kuwatenganisha wavulana pacha waliokuwa wameungana katika kichwa.

Kwa mujibu wa madaktari, wavulana hao wenye umri wa miaka miwili ambao ni Jaga na Kalia walifanyiwa upasuaji uliochukua takriban saa 16 na sasa wako katika chumba wagonjwa mahututi (ICU) katika taasisi ya matibabu na sayansi ya All India.

Hata hivyo, mapacha hao walizaliwa wakiwa wanatumia mishipa ya damu ya pamoja mbali na tishu za ubongo, hali isio ya kawaida ambayo hutokea mara moja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa.

Pamoja na mambo mengine, Mkurugenzi wa hospitali hiyo Randeep Guleria, aliviambia vyombo vya habari vya India kwamba siku 18 zijazo zitakuwa muhimu ili kuthibitisha ufanisi wa upasuaji walioufanya.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

WATOTO PACHA WALIOUNGANA VICHWA WATENGANISHWA INDIA