Watoto 400 wapotea ndani ya miaka mitatu

0
485

 

 Na Aziza Masoud, Dar es Salaam


WAKATI matukio ya upotevu wa watoto yakiendelea kushika kasi katika maeneo mbalimbali nchini,  imebainika ndani ya miaka mitatu watoto 399 wamepotea katika maeneo mbalimbali nchini.

Matukio hayo ni yale tu yaliyoripotiwa vituo vya polisi katika mikoa mbalimbali kati ya Januari mwaka juzi hadi Agosti mwaka huu.

Takwimu ambazo MTANZANIA limepewa na polisi makao makuu, zinaeleza kati ya watoto hao waliopotea wa kiume ni 238 na wa kike 161.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa, aliliambia MTANZANIA jana kuwa sababu kuu za kupotea kwa watoto ni imani za kishirikina, kulipiza visasi, kujipatia kipato na uzembe wa wazazi ama walezi.

“Kwa kipindi cha mwaka 2016 watoto 186 waliibwa, kati ya hao wanaume ni 114 na wanawake 72.

“Mikoa iliyoongoza kwa wizi huu katika mwaka huo ni Dar es Salaam watoto 23 (Temeke 13, Kinondoni 10) na Shinyanga watoto 22,” alisema Mwakalukwa.

Alitaja mikoa mingine kuwa ni Mkoa wa Mara watoto 16, Mbeya 15 na Morogoro 13.

Kwa mujibu wa Mwakalukwa, mwaka jana watoto 134 waliibwa. Kati ya hao wanaume ni 79 na wanawake 55 na mkoa ulioongoza kwa matukio hayo ni Dar es Salaam watoto 23 (Kinondoni 13, Ilala sita na Temeke wanne).

“Mkoa uliofuata kwa kuibwa watoto ni Kilimanjaro ambako kuliripotiwa kuibwa watoto 15, Manyara 13 na Shinyanga 11,” alisema Mwakalukwa.

Alisema kwa mwaka huu, katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti watoto walioripotiwa kuibwa ni 79 ambao kati yao wanaume ni 45 na wanawake 34.

Alitaja mikoa iliyoongoza kwa mwaka huu ni Mwanza watoto 11, Geita wanane na Dar es Salaam wanane (Ilala watano, Kinondoni watatu).

Alisema kati ya watoto 399 walioibwa, 209 walipatikana. Mwaka juzi walipatikana 91, mwaka jana 71 na mwaka huu 47.

 

WATUHUMIWA WALIOKAMATWA

Takwimu hizo zinaonesha watuhumiwa 186 wa wizi wa watoto hao walikamatwa katika kipindi cha miaka mitatu.

Mwakalukwa alisema kwa mwaka juzi walikamata watuhumiwa 81 waliohusika na matukio hayo, mwaka jana 65 na mwaka huu 40.

Alisema kutokana na matukio, hayo Jeshi la Polisi limekuwa likichukua hatua mbalimbali kupambana na uhalifu huo na kuhakikisha vitendo hivyo haviendelei.

“Jeshi la Polisi limejipanga kimkakati kuhakikisha linadhibiti vitendo hivi dhidi ya watoto, hususani wizi wa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here