Imechapishwa: Fri, Aug 25th, 2017

WATOTO 30 KUFANYIWA UPASUAJI WA VICHWA

Na MARGRETH MWANGAMBAKU (TURDACO)

-DAR SE SALAAM

WATOTO 30 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi, wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI).

Akizungumza na MTANZANIA Ofisa habari wa MOI, Patrick Mvungi, alisema upasuaji huo unatarajia kufanyika Agosti 26, mwaka huu.

“Tunashukuru tunaendelea kupata ufadhili kutoka kwa ndugu zetu wa Jumuiya ya Waumini wa madhehebu ya Shia,” alisema Mvungi.

Alisema waumini hao wamekuwa wakijitolea fedha, damu na vifaa tiba kwa ajili ya upasuaji huo.

Alisema meza tatu zitatumika ambapo kila moja inatarajiwa kufanya upasuaji watoto 10

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

WATOTO 30 KUFANYIWA UPASUAJI WA VICHWA