29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wateja wa hoteli wapewa ‘bunduki’ kuwakabili ndege wasumbufu

PERTH, AUSTRALIA

WAKATI baadhi ya hoteli katika majiji yaliyopo pwani kama vile Dar es Salaam yakikabiliwa na kero kutoka kwa kunguru wasumbufu, hoteli moja nchini Australia imevumbua njia ya kuzuia ndege wasumbufu kusumbua wageni wake.

Kwa mujibu wa mashirika ya habari, hoteli iliyo katika mji wa Perth, huwapa wageni wake bunduki bandia za kurushia ndege wa baharini maji ili kuwafukuza wanapokula ufukweni.

Mmiliki wa hoteli hiyo ya 3Sheets, Toby Evans, anasema ndege hao wa baharini wanaoitwa ‘seagulls’ husumbua wageni hivyo akaamua kutafuta njia ya kuwafukuza.

Awali ndege hao walikuwa wakisubiri wateja wamalize kula na kufuatilia makombo, lakini kadiri muda ulivyozidi kwenda wakaanza tabia ya kudonoa vyakula vikiwa mikononi mwa wateja.

Hivyo, ubunifu wa kutumia bastola za maji umesaidia kupunguza tatizo hilo kwa kiasi kikubwa.

Evans anasema kabla ya ubunifu huo, alitumia mabomu feki ya kielektroniki pamoja na bundi feki, lakini ni bastola ndizo zilizoweza kufanya kazi ipasavyo.

Inasemekana kila meza huwekewa bunduki hizo za maji na sasa wateja wameridhishwa na uwezo wake wa kuwafukuza ndege hao kwa njia ambayo pia huwaburudisha.

Bila shaka, wawekezaji katika sekta ya utalii katika majiji kama Dar es Salaam wanaweza kuiga mbinu hii au wavumbue mbinu nyingine bora zaidi.

Mbinu hizo zitaua ndege wawili kwa jiwe moja; si tu kukabiliana na kunguru wakorofi bali pia kufurahisha wageni, kitu ambacho kitawaongezea mapato kwani wateja wengi wanaweza kufurahishwa na kufika kwa ajili hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles