27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania waaswa kufanya kazi kwa uadilifu

pengoNa FERDNANDA MBAMILA-DAR ES SALAAM

WATANZANIA wameaswa kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu, weledi na uzalendo ili wapate heshima na kuthaminiwa na jamii inayowazunguka kwa kutambua mchango wao katika taifa.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo alisema hayo  Dar es salaam juzi  wakati wa hafla ya kukabidhiwa nishani ya Benemerenti (anayestahili), kwa Padri Dk. Fredrick Kigadye.

Nishani hiyo hutolewa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kulitumikia kanisa na jamii kwa ujumla.

Askofu Pengo alisema Baba Mtakatifu ametambua uadilifu wa mtu katika kuwatumikia wananchi kwenye shughuli za jamii, hivyo basi wanapaswa kumuunga mkono kutokana na uamuzi wake.

“Ni vema tukatambua  kwamba kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio mahali popote pa kazi na katika maisha yetu ya kila siku,” alisema Kardinali Pengo.

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki Iringa, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, alisema Dk. Kigadye amekuwa katika baraza hilo kwa muda wa miaka 35 huku akifanya kazi katika Idara ya Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa mafanikio makubwa.

“Dk. Kigadye ameonyesha ni namna gani watu tunapaswa kujitoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu kupitia vipawa na taaluma walizojaliwa na Mwenyezi Mungu, hii inatia moyo sana,” alisema Askofu Ngalekumtwa.

Naye Dk. Kigadye alisema anajisikia mwenye furaha na wa thamani kwa kupewa tuzo ya heshima na kiongozi mkubwa duniani.

Alisema  tuzo hiyo inamuongezea chachu ya kuishi katika misingi imara ya maadili na weledi.

“Nitumie fursa hii kutoa rai kwa Watanzania wengine hasa baraza la Walei wa Kanisa Katoliki nchini kutekeleza majukumu yao kwa kujituma zaidi   kuwahudumia wanajamii wanaohitaji huduma za kanisa ikiwamo elimu na afya,” alisema.

Padre Dk. Kigadye amekuwa Mtanzania wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo baada ya  Papa Francis kukubali maombi ya TEC ya kumtunuku tuzo ya heshima aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Afya Mstaafu wa Baraza hilo, Dk. Kigadye kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa Kanisa Katoliki na baraza akiitumikia idara hiyo na majukumu mengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles