27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania ruksa kujiunga jeshi la Uingereza

LONDON, UINGEREZA



RAIA wa kigeni kutoka mataifa ya Jumuiya ya Madola ambayo Tanzania ni mwanachama, wataruhusiwa kujiunga na Jeshi la Uingereza hata kama hawajawahi kuishi nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Baraza la Mawaziri la Uingereza, hiyo ni sehemu ya mkakati unaolenga kukabiliana na uhaba wa askari  wapya nchini humo.

Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo  inatarajia kutangaza kuwa waombaji wapya jeshini kutoka nchi za Jumuiya ya Madola kama vile Australia, India, Canada, Kenya na Fiji si lazima wawe wameishi Uingereza kwa miaka mitano kama ilivyokuwa awali.

Kwa mujibu wa  sera hiyo, waombaji watafikiriwa kujiunga na majeshi yote ikiwamo lile la wanamaji (Royal Navy) na anga (RAF) huku maombi mapya yakitarajiwa kutangazwa mapema mwaka 2019.

Serikali inatarajiwa kuwa mabadiliko hayo yatasaidia kupatikana askari wa ziada 1,350 kujiunga na jeshi la nchi hiyo kila mwaka.

Jeshi litaanza mchakato wa kusajili mapema mwaka ujao, wakati Royal Navy na RAF yatakapoanza mchakato mara moja kuanzia sasa.

Maombi kutoka raia wa nchi zilizo nje ya Jumuiya ya madola hayatapokelewa, ilisema taarifa hiyo.

“Askari wa kigeni na Jumuiya ya Madola kwa historia wamekuwa sehemu muhimu ya Jeshi la Uingereza na hivyo ninakaribisha ongezeko lao kwa idadi yenye ukomo,” Mark Francois, mmoja wa wajumbe wa kamati ya uteuzi ya ulinzi, aliliambia Gazeti la Daily Telegraph, ambalo lilikuwa la kwanza kuchapisha taarifa hiyo.

Majeshi ya Uingereza yana upungufu wa askari wa nchi kavu,  wanamaji na anga 8,200, kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa mapema mwaka huu, ukiwa ni upungufu mkubwa zaidi tangu mwaka 2010.

Francois alieleza sababu za jeshi kukosa askari wapya kuwa ni pamoja na kiwango cha juu cha ajira, ukubwa wa kizazi kilichozeeka.

Pia alisema ongezeko la unene na idadi ya watu Weusi, Waasia na wengineo ambao hawana uwezekano wa kuomba kazi ya jeshi kuwa sababu nyingine ya hali hiyo.

Francois alipendekeza ziwepo hatua za makusudi kuwavutia zaidi Weusi, Waasia na makundi mengine ya jamii ndogo jeshini,  bila kusahau wanawake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles