24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania changamkieni fursa vyuo vya nje

Christina Gauluhanga -Dar es Salaam

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ya kusoma vyuo vya elimu ya juu nje ya nchi ili kupata ujuzi  unaoendana na mabadiliko ya haraka ya teknolojia.

Wito huo umetolewa mwishoni wiki na mwambata mwenza  wa Taasisi ya Elimu ya Juu ya Edugate ya nchini Uingereza,  Aliyuthuman Sadhique wakati wa uzinduzi wa programu maalumu ya kusaidia wanafunzi katika nchi zenye uchumi wa kati inayofahamika kama LICAP.

Sadhique alisema programu hiyo inalenga kuwafikia wanafunzi na wahitimu mbalimbali kutimiza malengo katika vyuo maalumu vilivyopo Uingereza na Sri Lanka.

“Edugate kwa kushirikiana na Taasisi ya British College of Applies Studies ya Sri Lanka, tumedhamiria kuwekeza  katika elimu hapa nchini, hususan kuwawezesha Watanzania kwenda kusoma nje ya nchi, ikiwamo kuwasaidia  kimasomo,” alisema Sadhique.

Alisema wamezindua programu hiyo ambayo itaaendana na  kongamano maalumu litakalotoa fursa kwa Watanzania kuzitambua fursa hizo za elimu.

Aliwataka wale wote wenye nia ya kusoma nje ya nchi kuhudhuria kongamano hilo na kwamba litakuwa na faida kubwa hususan kwa wahitimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano (IT), usimamizi wa fedha, uhandisi na taaluma zingine.

Alisema kwa wale ambao ufaulu wao utaonekana kuwa ni wa juu, watasaidiwa kupata udhamini kupitia programu hiyo  ya LICAP. Mmoja wa waratibu wa kongamano hilo, David Munanka, alisema mafunzo hayo yamekuja wakati mwafaka ambao Serikali ya awamu ya tano inatekeleza dira yake ya kuelekea uchumi wa viwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles