25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘Watanzania changamkie fursa EAC’

makongoro nyerereNa Florian Masinde, Dar es Salaam

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Makongoro Nyerere, ambapo alisema nchi za Afrika Mashariki zinashirikiana kwa mambo mbalimbali ikiwamo Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja, Umoja wa Fedha na Shirikisho la Kisiasa.

Alisema kupitia makubaliano hayo, Watanzania wana nafasi ya kwenda kufanya baishara katika nchi nyingine bila kuzuiwa, na hivyo kuwa na nafasi ya kusambaza biashara zao katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Huu ni muda wa Watanzania kuchangamkia nafasi zilizopo za kufanya biashara kwa nchi za Afrika Mashariki, vikwazo vilivyopo kwa sasa ni wananchi wengi wa Afrika Mashariki bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu hilo, lakini tumejipanga katika hilo,” alisema Makongoro.

Alisema kwa kutambua changamoto hiyo ya wananchi wengi kutokufahamu nafasi hiyo, wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania wataendesha programu ya kuwaelimisha Watanzania jinsi wanavyoweza kunufaika na ushirikiano huo.

Makongoro alisema programu hiyo ilianza Aprili 4 na itafanyika hadi Aprili 23 ambapo kwa kuanza wamepanga kukutana na Kamati za Bunge, Taasisi za Elimu ya Juu, vyombo vya habari, kutembelea soko la Kariakoo na soko la Samaki la Feri.

Naye Mbunge wa EALA, Shyrose Bhanji, alisema kuna fursa nyingi ambazo Watanzania wanapaswa kuzichangamkia, hasa kupitia Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja.

“Watanzania hawajui kuwa bidhaa hazina kodi baada ya kuondoa ushuru wa forodha kwa nchi wanachama kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya Jumuiya, hivyo wanatakiwa kutambua na kupeleka bidhaa zao na kujitahidi kuwa karibu na wengine ili kuweza kupata nafasi ya kuzitumia fursa hizo,” alisema.

Wabunge hao walielezea fursa muhimu kwa sasa ambayo Watanzania wanatakiwa kuichukulia kwa uzito, ambayo ni  walimu na wataalamu wa lugha ya Kiswahili kwenda kutafuta ajira ndani ya Jumuiya kutokana na nchi wanachama kuanza kufundisha somo la Kiswahili katika nchi zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles