25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Watalaamu wa mazingira badilikeni-Makamba

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya  Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  January Makamba amewataka wataalamu elekezi wa tathmini ya athari kwa mazingira  kubadilika katika utendaji    tasnia hiyo iendelee kukua na kutoa mchango stahiki katika maendeleo ya taifa.

Hayo aliyasema  Dar es Salaam mwishini mwa wiki, wakati akifungua mkutano wa pili wa mwaka wa Chama cha Wataalamu Elekezi wa Tathmini Athari za Mazingira, ukaguzi na vibali vya awali.

Alisema   wataalamu hao wana umuhimu mkubwa katika ujenzi wa uchumi, lakini lazima wabadilike namna ya utendaji wao wa kazi.

“Katika changamoto  za namna ya ufahamu na  kufanya wa tathimini na ukaguzi wa mazingira nyie kama chama  mna uwezo wa kujipanga  kuanzisha  programu za mafunzo na kubadilishana uzoefu  kwa kufanya hivo itasaidia kuboresha na kuimarisha uwezo wenu wa katika utendaji,’’  alisema Makamba.

Alisema suala la  tathimini za athari kwa mazingira linapewa kipaumbele  kwenda sambamba na azma  ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Kati na Viwanda ifikapo mwaka 2025.

“Kuna changamoto kadhaa kwenye usajiri wa  wataalam elekezi  wa mazingira  kuhusu ulipwaji wa ada za mwaka ambako serikali inapoteza mapato  yake.

“Taarifa ya NEMC inaonyesha   mwaka 2018 wataalam binafsi wanadaiwa Sh milioni 600 na makampuni yanadaiwa Sh  milioni 250 kama ada za mwaka,” alisema.

Alisema serikali inawatambua wataalam na kazi zao kwa wale wasiolipa ada za mwaka katika tasnia hii walipe mara moja kabla hatua kali za sheria hazijachukuliwa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Baraza la Taifa  Usimamizi wa Mazingira (NEMC),  Vedast Makota alisema Baraza limejipanga kufanya  marekebisho kwenye  kanuni ya tozo na ada pamoja  na kanuni ya  tathimini athari  kwa mazingira..

Dk. Makota alisema  hadi kufikia mwezi wa nne mwaka huu, NEMC iliweza  kutoa  kanuni mpya ya ada na tozo ya baraza  ambayo kimsingi  ilizingatia malalamiko ya wananchi  ambao walikuwa wanatozwa katika ada na tozo mbalimbali.

“Hapo awali miradi ilikuwa inatozwa kwa  asilimia ya gharama  ya uwekezaji  lakini kwa sasa tumeliondoa  na  kuweka viwango ambavyo vitakuwa  rafiki kwa  wawekezaji,’’ alisema Dk. Makota.

Alisema kwa sasa miradi midogo  inatozwa kuanzia milioni mbili tofauti na hapo  awali ilikuwa inatozwa kuanzia milioni 10 ambako miradi ya serikali inatozwa Sh milioni 50  kulingana na  gharama za uwekezaji wa mradi lakini ilikuwa Sh milioni 500 hadiSh milioni 600.

Dk. Makota alisema kanuni mpya walizozitoa Septemba  mwaka huu  kwa upande wa sekta ya viwanda, mwekezaji anaruhusiwa kuomba kibali hata kama hajakamilisha matakwa ya msingi kwenye  andiko la awali  ambako masharti yanamtaka  kuwa ndani ya miezi minne awe amepata cheti.

Mwenyekiti wa  Chama cha Wataalam Elekezi wa  Mazingira Tanzania, Profesa Hussein Sosovele, alisema  kama chama  kimejipanga kufanikisha  azma ya serikali ya kufikia  uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025 kwa  kufanya uchambuzi yakinifu  juu ya tathmini ya uwekezaji na kuainisha namna uwekezaji huo utakavyoleta tija bila kuharibu mazingira.

“Chama kitaishauri serikali juu ya namna  bora ya kutumia  rasilimali bila kuharibu mazingira kwa kiasi ambacho hakitaweza  kurekebishika,’’ alisema Prof. Sosovele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles