27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

WATAFITI WA KILIMO JIBUNI HOJA ZA WAKULIMA

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA


TAASISI za utafiti wa kilimo nchini, zimetakiwa kufanya kazi za kitafiti zinazojibu hoja za wakulima na jamii badala ya kupata vyeti.

Agizo hilo limetolewa jana na Waziri wa Kilimo, , alipokuwa akifungua maonyesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki (EAGC) kwa ushirikiano na Kituo cha Utafiti cha Selian Arusha.

Maonyesho hayo yalikutanisha wakulima zaidi ya 4,000 yakilenga kukuza ubunifu wa viwanda, biashara, usalama wa chakula na lishe kupitia mageuzi ya kilimo biashara.

Akizungumza na wakulima pamoja na wadau mbalimbali, Dk. Tizeba alisema mpaka sasa hakuna utafiti wa moja kwa moja kati ya wakulima na watafiti kwa kuwa kila mmoja anafanya shughuli zake bila kumshirikisha mwenzake.

“Ukienda vituo vya utafiti, utaona wanachofanya ni tofauti na maeneo walipo wakulima. Kwa hiyo, watafiti wa kilimo nawaagiza tafiti mnazofanya, lazima zijibu hoja za wakulima na si kupata vyeti.

“Tafiti ni pamoja na kujibu changamoto zinazomzunguka mkulima na jamii, kwamba kupitia mlichotafiti, mnawezaje kusaidia wakulima kupata pembejeo kwa wakati na bei nzuri,” alisema Dk. Tizeba.

Akijibu maswali ya wakulima baada ya kutembelea mashamba darasa na vibanda vya maonyesho, Dk. Tizeba alitumia fursa hiyo kuelezea juu ya masoko na kukanusha uvumi unaosema maharage ya soya yana ugonjwa.

“Taarifa hizo hazina ukweli na Serikali inaendelea kufanya uchunguzi kwa aliyezisambaza na tukipata ushahidi na kumkamata, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wakulima wa Mpunga Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, Ndilana Mahona, alisema mpunga umewawezesha kupata mafanikio zaidi tofauti na awali kwa kuwa wanalima kisasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles