30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WATAALAMU WA SILAHA ZA SUMU KUINGIA SYRIA LEO

THE HAGUE, UHOLANZI


MAOFISA wa Urusi wamesema wataalamu wa kimataifa wa kudhibiti silaha za kemikali (OPCW) wanatarajiwa kuwasili Douma leo kuchunguza madai ya uwapo wa shambulizi la sumu katika mji huo wa Syria.

Hatua hiyo inakuja huku Marekani ikieleza wasiwasi wake kuwa huenda Urusi tayari imeshaharibu ushahidi eneo la tukio.

Ofisa Mwandamizi katika Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Igor Kirillov alisema; “Tunapanga ziara ya wataalamu wa OPCW ifanyike siku ya Jumatano (leo) kwa hiyo Urusi haizuii wachunguzi wa kimataifa kuzuru Douma kwa njia yoyote ile,” alisema Kirillov.

Awali Marekani iliilaumu Urusi kwa kuwazuia wachunguzi hao kufika katika eneo kulikofanywa shambulizi linalodaiwa kuwa la kemikali na imesema huenda Urusi au Syria zimeshaharibu ushahidi.

Lakini Balozi wa Urusi katika OPCW, Alexander Shulgin alikana madai hayo na kusema nchi za Magharibi hazitaki uchunguzi kwa kuwa zimeshafanya maamuzi yao wenyewe.

“Labda wanaogopa baada ya wataalamu hao kufanya uchunguzi watapinga uwapo wa shambulizi la sumu jambo ambalo lilikuwa kisingizio cha mashambulizi yaliyofanywa na Marekani, Ufaransa na Uingereza dhidi ya Syria, ambayo haikuweza kujitetea,” alisema Shulgin.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamekosolewa na wapinzani wao wa kisiasa kutokana na maamuzi yao ya kushiriki katika mashambulizi dhidi ya Syria.

Lakini May alijitetea mbele ya bunge na kupata uungwaji mkono kwa uamuzi wake.

“Wacha niwe muwazi kabisa. Tumeshambulia kwasababu ni jukumu letu la kitaifa. Ni jukumu letu la kitaifa kuzuia kutumika kwa silaha za kemikali nchini Syria na kulinda maelewano ya dunia nzima kwamba silaha hizi hazistahili kutumika,” alisema May.

“Hatuwezi kukubali silaha za kemikali kufanywa kuwa jambo la kawaida iwe ni nchini Syria, katika mitaa ya Uingereza au mahali pengine kokote duniani,” aliongeza kiongozi huyo wa Uingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles