25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WASTAAFU WAISHAURI SERIKALI UHAMISHO WALIMU WA SEKONDARI KWENDA MSINGI

Eliud Ngondo, Mbeya

Baadhi ya Wadau wa Elimu mkoani hapa, wameishauri Serikali kupitia upya utaratibu wa kuwahamisha walimu waliokuwa wanafundisha shule za sekondari kwenda kufundisha shule za msingi.

Wamedai kitendo hicho kinaweza kusababisha mfumo mzima wa elimu nchini kuharibika kutokana na maandalizi hafifu.

Wakizungumza katika mkutano jana, wadau hao wakiwamo wazee wastaafu wamedai wameanza kupata malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa shule za msingi kuwa wanashindwa kuwaelewa walimu wao wapya tofauti na waliokuwa wanawafundisha awali.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wastaafu Wilaya ya Mbeya, Mwalimu Erick Mwaituka,  amesema lengo la serikali kuwahamisha walimu hao kutoka shule za sekondari kwenda za msingi ni zuri lakini lilitakiwa maandalizi ya kutosha.

“Lengo la Serikali ni zuri sana maana inalenga kupunguza tatizo la upungufu wa walimu kwenye shule za msingi, lakini sisi tunashauri ingeangalia mfumo mzima wa elimu ya nchi yetu vinginevyo tunaweza tukajikuta tunazalisha changamoto nyingine badala ya kuzipunguza,” amesema Mwalimu Mwaituka.

Naye mstafu Wilson Mwanguku, amesema baadhi ya walimu walio na elimu ya shahada wanaweza kusababisha changamoto kwa kutumia mfumo wa ufundishaji wa sekondari kwenye shule za msingi hali ambayo inaweza kuhatarisha uelewa wa watoto.

“Mwalimu aliyekuwa amezoea kufundisha Sekondari na alikuwa ameanza baada ya kupata shahada ni vigumu kumfundisha mtoto wa shule ya msingi kwa ufanisi na hivyo kuna hatari watoto kutoelewa vizuri masomo,” alisema Mwanguku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles