31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wasanii wa Bongo mnakoelekea siko

DSCN7737babay jayLINNNDSCN8002NA FESTO POLEA

WAKATI juhudi za kupata vazi la Taifa zikiendelea, kuna haja ya kuanzishwa mchakato wa kupata vazi la wasanii ili wawe wakilitumia wakiwa jukwaani.

Sina maana kwamba, wasanii hao wachaguliwe mavazi ya kuvaa wawapo stejini bali wawekewe kikomo cha mavazi, muda wa kuvaa, mazingira na hadhira iliyopo.

Naandika hili kwa kuwa kuna kila dalili ya wasanii wetu kufikia hatua ya kuiga aina ya mavazi wanayovaa wasanii wa Magharibi ambapo mara kwa mara huwa stejini nusu utupu akiwemo, Robyn Rihanna Fenty (Rihanna), Miley Ray Cyrus (Miss Cyrus), Onika Tanya Maraj (Nicki Minaj), Beyonce Giselle Knowles-Carter (Beyonce), Stefani Joanne Angelina Germanotta (Lady Gaga) na wengine wengi.

Wasanii hawa wana vipaji vingi, nadhani itakuwa vema kama mtaiga fani zao zikiwemo uigizaji, uonyeshaji mavazi ya makampuni mbalimbali yanayowaingizia kiasi kikubwa cha fedha na namna wanavyotumia sauti zao kuimba nyimbo nzuri lakini si kuiga aina ya mavazi wanayovaa wakiwa stejini kwa sababu hayana maadili na faida yoyote katika majukwaa yetu.

Waigizaji hawa ndio wanaotangazwa zaidi kwa uvaaji wa mavazi ya nusu uchi wakiwa stejini na katika mapumziko ya maisha yake halisi huku Lady Gaga akiweka historia ya kutapika mara nne akiwa stejini baada ya kupanda akiwa mgonjwa.

Licha ya mavazi yao pia aina ya uchezaji wao na wanaocheza nao ingawa yanawaongezea jina lakini kwa hapa yanaweza kupunguza mashabiki na kuongeza pia kwa wakati mmoja.

Lady Gaga aliyezaliwa Machi 28, 1986 huko Mnhattan New York licha ya kuwa mwimbaji ni mwandishi wa nyimbo, prodyuza, mwigizaji na pia anajihusisha na harakati za utoaji misaada kwa watu wenye uhitaji maalumu. Huyu naye awapo jukwaani hujichetua kwa aina ya unenguaji wake na mavazi anayovaa huwa yakionyesha sehemu kubwa ya mwili wake ambao si vizuri kuigwa na wasanii wetu.

Muigeni Miss Cyrus uwezo wake wa kupiga kinanda, gitaa pamoja na kuimba muziki wa Pop, mwanamuziki huyu aliyezaliwa Novemba 23, 1992 katika mji wa Los Angeles, California nchini Marekani, pia ni mwandishi wa nyimbo mbalimbali, mwimbaji na mwigizaji, lakini awapo jukwaani ni kichaa wa nguo za nusu utupu na aina ya unenguaji wake pia si wa kuigwa na wasanii wetu.

Beyonce, aliyezaliwa Septemba 4, 1981 huko Houston, Texas na sasa anaishi Los Angeles, California licha ya kuwa mwanamuziki ni mwandishi wa nyimbo, prodyuza wa muziki, mwigizaji, mnenguaji na pia ni mfanyabiashara. Anafanya muziki wa R&B, Pop na Soul, pia naye ni mfuasi mkubwa wa nguo zinazoacha ama kuonyesha eneo kubwa la mwili wake.

Nicki Minaj amezaliwa Desemba 8, 1982 huko Saint James visiwa vya Trinidad na Tobago, ni mwanamuziki wa hip hop, R&B na Pop, anaandika, anaimba na anarap, huyu naye ni mfuasi wa nguo zinazoacha wazi ama kuonyesha eneo kubwa la mwili wake naye pia si wa kuigwa.

Rihanna amezaliwa Februari 20, 1988 huko Saint Michael, Barbados ni mwimbaji, mwigizaji na pia ni mwanamitindo anapenda kuimba R&B, Pop, Reggae, hip hop, dance-pop na Soul. Ndiye anayefanya muziki wa aina nyingi kuliko wenzake hao, huyu naye huwa na tabia ya kuvaa nguo zinazoacha wazi ama kuonyesha sehemu kubwa ya mwili wake jambo ambalo si zuri kuigwa na wasanii wetu.

Nguo fupi (vimini), nguo zinazobana na kuonyesha maungo yao zilikuwa zikionekana kwa wanenguaji wa muziki wa dansi ambao kwa kiasi fulani wamejaribu kuondokana na hali hiyo iliyopigiwa kelele na wadau mbalimbali wa muziki huo ingawa haijaisha kwa baadhi ya bendi za muziki huo.

Hali hiyo ikaja kuonekana kwa waigizaji wa filamu za Bongo ambapo baadhi ya waongozaji na maprodyuza wakidai kwamba baadhi ya wasanii hulazimisha kuvaa mavazi hayo tofauti na hivyo hukataa kuigiza katika filamu zao huku wengine wakidai linatokana na uhitaji wa soko la filamu.

Sasa limehamia kwa waimbaji wetu wa muziki pendwa wa Bongo Fleva hasa wakiwa stejini, wanaume hudai wamepandwa na mzuka wa kuvua nguo na kuonyesha nguo zao za ndani, vifua vyao na wanawake nao wakitoa sababu mbalimbali ikiwemo ya kuwavuta mashabiki katika onyesho lao, kibiashara, kuwa huru na kunogesha shoo zao.

Nimeandika makala hii kwa kuwa wapo wasanii wa hapa nchini walioanza kuwaiga wasanii hawa katika baadhi ya maonyesho yao huvaa nguo zisizo na staa bila kujali hadhira iliyomzunguka katika onyesho hilo.

Na kwa kasi hii mnayoionyesha mtawafikia wasanii hao wa Magharibi kwa haraka mno na huenda mkawazidi nao wakaja kuwaiga kama video za nyimbo zenu za maonyesho yenu hazitapata nafasi ya kuonyeshwa katika vituo vya runinga vilivyopo nchini kwao

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles