24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wasabato watenga milioni 100 za kupambana na corona

AVELINE  KITOMARY, DAR ES SALAAM

Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania kupitia mradi wake wa Maendeleo na Misaada wakati wa maafa (ADRA) imetenga kiasi cha Sh. million 100  kwaajili ya kununua vifaa kinga ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana ya maambukizi ya virusi vya corona(Covid-19).

Akizungumza leo Ijumaa Mei 29, jijini Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadvesta Wasabato Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania, Mark Malekana amesema vifaa vitatolewa katika hospitali za serikali  katika Mikoa mbalimbali kote nchini.

Askofu Malekana amesema mpaka sasa wamefiki zaidi ya asilimia 10 ya ugawaji wa vifaa hivyo ambapo wametoa mikoa ya Dar es Salaam na Arusha na ifikapo Disemba mwaka huu zoezi hilo litakamilika.

“Kanisa kupitia Shirika la Maendeleo na Misaada wakati wa maafa (ADRA) limejizatiti kushirikiana na serikali katika kupambana na virusi hivi vya Corona na tumekuwa tukitoa misaada mara kwa mara mfano tulitoa Arusha na leo tumetoa hapa wilaya ya Temeke,

“Leo tumetoa glops, Vitakasa mikono boksi 182, mask boksi 45 na vitu hivyo vimegharimu na thamani ya shilingi milioni 8” amesema

Pia amesema vifaa ambavyo wamekuwa wakivitoa vimekuwa vikitengenezwa hapa nchini lakini pia wamekuwa wakitoa elimu ya namna gani ya kujikinga na maambizi hayo.

Amesema utoaji wa vifaa hivyo hautabagua watu na imani fulani badala yake vitatolewa kwa watu wote wenye mahitaji ili kuisaidia nchini kupambana na janga hili.

“Sisi ni Watanzania na wote ni wamoja vifaa hivi tunavyotoa vitatumika na watu wote bila kujali imani zetu na tofauti zingine ,”ameeleza .

Askofu Marekana amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya corona na kufanya kazi kwa bidii.

“Namshukuru sana raisi wetu katika haya mapambano amefanya vizuri sana ,tumemtanguliza Mungu na tumneshinda  hata hivyo nawaambia watanzania wasibweteke waendelee kuchukua tahadhari za kifaya na waendelee kufanya kazi kwa bidii.

“Ninachokuomba hili viongozi waangali ni kuhakikisha kila mtu anapata nafasi ya kuambu kwa siku zao za ibada naomba viongozi wazingatie hili kusiwepo na vizuizi katika kuambu hasa kwa wanafuzi mfano kama na ijumaa,Jumamosi,Jumapili kila mtu apewe nafasi ya kuabu hasa kwa wanafunzi,”ameeleza Askofu Marekana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles