24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WANAWAKE MONDULI WAUNDA BARAZA LAO

Na MARY MWITA-MONDULI

WANAWAKE wa jamii za wafugaji wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha, wameanzisha baraza la wanawake ili liwasaidie kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Pia, wameunda baraza hilo liwasaidie kukabiliana na matatizo ya ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni, ubakaji na ukatili wa aina mbalimbali.

Mkurugenzi wa baraza hilo, Mary Morindat, akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo  mwishoni mwa wiki, alisema wanawake wa jamii za kifugaji nchini, wamekuwa waathirika wakubwa  wa mabadiliko ya tabia nchi.

Kutokana na hali hiyo, alisema baraza hilo litawasaidia kupata uelewa na kuchukua tahadahari dhidi ya mabadiliko hayo.

Kwa mujibu wa Morindat, wanawake wanaounda baraza hilo wanatoka katika vitongoji na katika ngazi mbalimbali za utawala wilayani hapa.

“Ingawa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo wazi kuwa kila mtu anapaswa kumiliki ardhi na mali, katika jamiii za wafugaji wanawake hawaruhusiwi kumiliki ardhi.

“Kwa hiyo, baraza hili limejipanga kuhakikisha usawa kati ya mwanamke na mwanamume unakuwapo katika umiliki wa ardhi na katika masuala mengine.

“Nasema hivyo kwa sababu wanawake watapewa mafunzo mbalimbali kuhusu haki ya kumiliki  ardhi pamoja na kupambana na ukatili wa kijinsia  ambao unaendelea kuwaaathiri wanawake wa jamii yetu,” alisema.

Kwa upande wake, Mratibu wa mradi wa kupambana na ukatili wa majumbani unaotekelezwa na baraza hilo, Elizabeth Lesitei, alisema wanawake wilayani Monduli wamelemewa na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa na wanaume.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles