28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake mashujaa walioshika nyadhifa ulimwenguni

Na FARAJA MASINDE

NIANZE kwa kuwapongeza wanawake wote duniani kwa kusherehekea siku yenu, tena hii leo ikiwa ni miaka mingi imepita tangu siku hii ilipoanzishwa rasmi huko nchini Marekani.

Kama inavyofahamika kwamba kwa hapa nchini maadhimisho ya kitaifa yanafanyika huko mkoani Simiyu, ambapo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Wakati sheherehe hizo zikitarajiwa kuendelea huko zilikopangwa, makala haya ni sehemu ya maadhimisho kwani  inaangazia wanawake ambao wamekuwa na ushawishi mkubwa kwenye siasa ulimwenguni.

Majina haya ya wanasiasa yamezidi kuwa makubwa na hata kuweza kuchuana na wanaume, hatua ambayo imeweza kuleta ushawishi hata kwa wanawake wengine kujikuta wakihamasika na uringo huo.

Ni jambo la kujivunia kuona kuwa Tanzania imekuwa ni miongoni mwa nchi zinazowaamini wanawake na kuwapa nafasi mbalimbali kwenye uongozi.

Hilo pia linathibitishwa na namna ambavyo wanawake wameshika nyadhfa mbalimbali za juu katika kuongoza mashirika na taasisi za umma, lakini kama hiyo haitoshi tunashuhudia hata kwenye baraza la mawaziri ambapo kumekuwapo kundi kubwa la wanawake hatua ambayo inatia moyo katika juhudi za kufikia usawa wa kijinsia.

Sasa hebu wafahamu wanawake hawa ambao wamekuwa na ushahwishi mkubwa kwenye nyanja ya siasa ulimwenguni na hata kutokea kuwa kivutio kwa wanawake wengi, hiyo ni kwa mujibu wa jarida maarufu ulimwenguni la Forbes ambalo limekuwa likichapisha matokeo ya tafiti mbalimbali.

Angela Merkel 

Angela Merkel 

Huyu ni Chancellor wa Ujerumani ambaye licha ya kutangaza kujiondoa kwenye maisha hayo ya kisiasa ifikapo mwakani, amekuwa ni shujaa wa taifa hilo kubwa barani Ulaya.

Ameitumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka tisa mfululizo ikiwa ni kipindi kirefu zaidi ikilinganishwa na waliowahi kutumikia wadhfa huo.

Amekuwa ni mwanamke mwenye nguvu kubwa na ushawishi wa kisiasa hatua ambayo imechochea kwa kiwango kikubwa kulifanya taifa hilo kuwa nafasi ya nne kwa uchumi mkubwa zaidi ulimwenguni na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) na kukifanya chama chake kuendelea kung’ara.

Christine Lagarde 

Christine Lagarde 

Ni mwanamke mpambanaji na mwenye nguvu kubwa ya ushawishi, anashika nafasi ya pili nyuma ya Angela Markel, amesogea nafasi hiyo kufuatia mwaka jana kufanyika kwa mageuzi kutoka kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na kuwa Rais wa Benki ya Umoja wa Ulaya (ECB).

Katika nafasi hiyo mpya, amewaza kutengeneza sera mpya za kifedha kwa mataifa 19 wanachama wa umoja huo, pia analenga kusimamia ukanda wa Ulaya ambao umekuwapo na changamoto za kiuchumi.

Nancy Pelosi 

Nancy Pelosi 

Huyu anashika nafasi ya tatu kwani awali alipotea kwenye orodha hii ya wanawake wenye ushawishi husasan kwenye nyanja ya siasa, lakini sasa amerejea hatua ambayo imechangiwa na kushika wadhfa wa Spika wa Bunge la Marekani.

Pia umaarufu wake ulichangiwa zaidi na ushiriki wake katika kesi iliyokuwa ikimkabili Rais wa taifa hilo kubwa kwa uchumi duniani, Donald Trump.

Ursula von der Leyen

Ursula von der Leyen

Hili ni ingizo jipya katika orodha hii, Leyen amechaguliwa kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Tume ya Ulaya ambayo ndiyo mwongozo wa Umoja wa Ulaya (EU).

Akiwa mwanamke wa kwanza kushika wadhfa wa urais, aliahidi kutumia baraza lake kuhakikisha analeta usawa wa kijinsia, ambapo kwasasa kwa kiwango kikubwa kumekuwapo usawa wa kijinsia ikiwa ni mara ya kwanza kwa historia ya baraza hilo.

Hii ina maana kwamba ameweza kumuondoa Theresa May’s baada ya kujiuzulu nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza kufuatia sekeseke la nchi hiyo kutaka kujiondoa katika Umoja wa Ulaya (EU).

Nicola Sturgeon

Nicola Sturgeon

Huyu ni waziri wa kwanza wa Scotland huku akiwa ni kiongozi wa chama cha Scottish National Party tangu mwaka 2014, amekuwa ni mwanamke mwenye mchango mkubwa kwenye serikali ya Scotland na hata kufanya kuwapo kwa usawa nchini humo.

Nirmala Sitharaman

Nirmala Sitharaman

Pamoja na kwamba suala la usawa wa kijinsia limekuwa ni kitendawili kwa taifa la India, lakini kwa mara ya kwanza Sitharaman ameweza kuvunja mwiko huo kwa kuwa waziri wa kwanza wa Fedha na Ushirikiano, ikikumbukwa kuwa India ni miongoni mwa mataifa yenye uchumi mkubwa duniani.

Wengine ni Jacinda Ardern, Queen Elizabeth II, Tsai Ing-Wen na Ivanka Trump.

Hata hivyo pamoja na orodha hiyo, wapo wanawake wengi ambao wamekuwa mashuhuri kwenye nyanja ya ushawishi wa kisiasa akiwamo, Hillary Clinton, mke wa rais mstaafu wa Marekani, Michelle Obama na wengine wengi.

Pamoja na orodha hiyo ya kimataifa, wapo pia wanawake ambao wamekuwa na ushawishi kwenye siasa za Afrika ambao ni pamoja na aliyekuwa Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, pia alikuwa ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais barani Afrika.

Sophia Abdi Noor, anatokea Kenya, ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa mbunge katika historia ya taifa hilo, alichaguliwa katika kaunti ya Isiolo, Kasikazini mwa Kenya, Agosti 2017.

Diane Rwigara, huyu anatokea nchini Rwanda, miezi kadhaa iliyopita aliweza kuleta changamoto kwa rais wa taifa hilo, Paul Kagame baada ya kutangaza adhma yake ya kutaka kuwania kiti cha urais.

Takwimu za UNWOMEN

Takwimu za shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wanawake (UNWOMEN) za mwaka 2019, zinaonyesha kuwa wabunge wanawake ni asilimia 24.3 tu kwenye mabunge yote ulimwenguni, likiwa ni ongezeko dogo kutoka asilimia 11.3 mwaka 1995.

Takwimu hizo zinaeleza kuwa hadi Juni 2019 ni wanawake 11 waliokuwa wakihudumu kuwa marais wa nchi huku 12 wakihudumu nafasi ya wakuu wa serikali.

Hata hivyo, Rwanda ndilo taifa lenye idadi kubwa ya wabunge wanawake wanaofikia asilimia 61.3 ya viti vyote bungeni.

Ulimwenguni kote kuna nchi 27 ambazo wanawake huzingatia asilimia chini ya 10.

Hata hivyo, takwimu za wabunge wanawake katika kila ukanda zinaonyesha kuwa katika nchi za Nordric, wabunge wanawake ni asilimia 42.5, Marekani asilimia 30.6, Ulaya ikijumlisha nchi za Nodric asilimia 28.6, Ulaya bila nchi za Nordric asilimia 27.2, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara asilimia 23.9,Asia asilimia 19.8, Umoja wa Falme za Kiarabu asilimia 19 na Pacific asilimia 16.3.

Wanawake wanaoongoza Serikali

Hadi kufikia Januari 2019, wanawake mawaziri walikuwa asilimia 20.7 tu, ambapo wizara tano maarufu walizokuwa wakiongoza ni pamoja na masuala ya jamii, ikifuatiwa na familia/watoto/wazee na walemavu. Nyingine ni mazingira, maliasili, nishati, ajira na biashara.

Hadi kufikia Februari 2019, ni nchi tatu tu zilizokuwa zimefikia asilimia 50/50 au zaidi ya wabunge bungeni ambazo ni Rwanda asilimia 61.3, Cuba asilimia 53.2 na Bolivia asilimia 53.1. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles