Wanaume watakiwa kujitokeza kupima saratani ya matiti

1
1232

Bethsheba Wambura, Dar es SalaamWanaume wametakiwa kujitokeza kupima saratani ya matiti kwenye Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), katika zoezi la upimaji saratani linaloendelea hivi sasa hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa takwimu, kati ya asilimia 100, asilimia moja inaonesha wanaume pia wako katika hatari ya kupata ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Meneja kitengo cha uchunguzi wa Saratani wa taasisi hiyo, Dk. Maguha Stephano, leo Jumanne Oktoba 9, akizungumza na Mtanzania Digital na kuongeza kuwa zoezi hilo litaendelea hadi Ijumaa Oktoba 12, mwaka huu.

Amesema hadi sasa zaidi ya watu 100 wameshafanyiwa vipimo na kupewa ushauri nasaha.

“Kila mwaka inapofika Oktoba ambao ni mwezi wa maadhimisho ya Saratani, ORCI inafanya upimaji wa Saratani ya matiti sambamba na utoaji wa elimu kwa wanawake ambapo mwaka huu tumeongeza kupima saratani ya mlango wa kizazi, saratani ya ini,  tezi dume na saratani ya ngozi kwa watu wenye albino.

“Hatutaki kuona wagonjwa wa Saratani wanaongezeka, tunajitahidi kufanya kazi kwa bidii kuona kama inaweza kuisha na tukishindwa hivyo basi angalau kupunguza ndiyo maana tunatoa huduma ya upimaji bure ili kila mtu apate nafasi ya kupima,” amesema.

Aidha, amesema mbali na kupima pia wanatoa elimu ya uchunguzi wa awali ambao mtu yeyote anaweza kujifanyia nyumbani na akigundua tatizo afike hospitali mara moja.

“Saratani ya matiti inashika nafasi ya pili kati ya saratani 10 zinazoongoza na zoezi hili ni endelevu hivyo mtu asipopata nafasi kwa sasa anaweza kuja hata baada ya zoezi kuisha,” amesema.

1 COMMENT

  1. Hakikisha Prof Mbaula kuwa kila Mkoa na eneo la kabila fulani wanafanya promotion kama priority ya utamaduni wao kimavazi kwa vifaa vya utamaduni. Ili huo utamaduni usife.Tuache kasumba kuwa unakwenda hoteli za Mikindani au Mtwara-Lindi au Mafia Island picha za utamaduni predominantly ni za kutoka Arusha. Mavazi mashuka ya makabila ya Arusha wakati Wamakonde, Wamwera wana utamaduni wao mkubwa. Sio mbaya kuonyesha picha na matangazo, vifaa vya utamaduni wa makabila mengine na kutangaza maeneo mengine ya utalii kila kona ili mgeni achague pa kwenda. Lakini ile ya kufukia tamaduni nyingine na kuzipa kipaumbele za Arusha hiyo muiangalie jamani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here