23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WANAUME CHANZO CHA ‘MKOROGO’ KWA WANAWAKE

Na TAUSI SALUM – DODOMA


BAADHI ya wanaume nchini wanatajwa kuwa kichocheo cha wanawake kutumia vipodozi vyenye viambata vya sumu ambavyo vimekuwa vikiwapa madhara ya ngozi.

Hayo yalielezwa Dodoma jana na Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati, Dk. Englibert Bilashoboka  alipozungumza na MTANZANIA.

Alisema wanawake wengi hutumia vipodozi hivyo kuwavutia wanaume ambao wamekuwa wakitamani wanawake wenye rangi nyeupe.

“Wanawake wengine hutumia vipodozi vyenye madhara katika ngozi zao wakati wakijua kuwa vimekatazwa na kujikuta wanapata madhara makubwa ya afya na kutumia gharama kubwa katika kujitibu,” alisema.

Alisema ingawa TFDA inafanya juhudi kubwa kuielimsha jamii juu ya madhara yanayotokana na matumizi ya vipodozi vyenye viambata vya sumu, mwitikio bado ni mdogo.

Dk. Bilashoboka alisema   vipodozi   na mvinyo vimekuwa vikichakachuliwa kwa kiasi kikubwa hivyo mamlaka kwa kushirikiana na raia imebaini kuwapo hali hiyo na kuanza kutumia mfumo wa ufuatiliaji wa bidhaa katika soko.

Hata hivyo, alitoa wito kwa wananchi kuwa makini kwa kuangalia taarifa kuhusu muda wa kuisha bidhaa wanazozinunua ili kulinda afya zao.

“Kutokana na mfumo wa ukaguzi ubora, hivi sasa mamlaka imeweza kudhibiti vipodozi bandia na hivi sasa kuna kesi mbili mahakamani zinazohusiana na vitu hivyo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles