23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WANASAYANSI WAGUNDUA SAYARI 10 MPYA

California, Marekani


SHIRIKA  la Masuala ya Angani la  Marekani (NASA) limetangaza kugundua sayari nyingine mpya 10 angani ambazo huenda zinaweza kusaidia uhai.

Wanasayansi kutoka NASA wanasema uchunguzi mpya wa darubini ya Kepler unaonyesha   sayari 10 zenye miamba ambazo zipo hatua chache kutoka kwa mkusanyiko wa nyota.

Sayari hizo   zote zipo nje ya jua katika mkusanyiko huo wa nyota.

Darubini hiyo ya Kepler sasa imegundua   sayari 50 katika maeneo tofauti yenye uhai angani.

Mwezi Februari mwaka huu NASA wakishirikiana na wanasayansi wa anga za mbali kutoka Uingereza na Ubelgiji, walifanya ugunduzi mkubwa wa sayari saba zenye ukubwa sawa na wa dunia ambazo zinaizunguka nyota mojawapo kama ilivyo kwa dunia kulizunguka jua.

Walibainisha kuwa sayari hizo saba  zinaizunguka nyota ijulikanayo kwa jina la Trappist One.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles