27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaomkwamisha Lukuvi kumaliza kero za ardhi waondolewe mapema

BENJAMIN MASESE – MWANZA

NI jambo la kufurahia pale unaposikia Watanzania wengi wakisifia serikali yao, hii ni ishara kwamba Rais Dk. John Magufuli, ameleta mabadiliko chanya katika utawala wake juu ya namna alivyowafikishia huduma katika maeneo yao au kutatua kero zao.

Ingawa ni vigumu kumridhisha kila mtu, lakini asilimia kubwa ya Watanzania wameridhishwa na  utawala wa Rais Magufuli ambaye hakika ameonekana kutokuwa na urafiki na mtumishi yeyote asiyeendana na kasi yake au kwenda kinyume na taratibu na maadili ya kazi.

Lakini, mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano yanatokana na wasaidizi wa Rais Magufuli ambao amekuwa akiwateua kushika nyadhifa mbalimbali na amekuwa hachelewi kuwaondoa pale wanapokengeuka. Jambo zuri zaidi ni pale anapomtumbua na kufafanua kosa lake ikiwa ni fursa kwa mwingine anayemrithi kwenda kurekebisha kasoro hiyo.

Ni jambo lisilo kificho kwamba Watanzania wengi walikuwa na matatizo yao katika sekta ya ardhi na kwa bahati nzuri, Rais Dk. Magufuli alifanya uteuzi wa mawaziri wake na kumuona Willian Lukuvi kama mwarobaini wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Hadi sasa hakuna anayebisha juu utendaji wa Lukuvi ukiangalia namna alivyosimama kidete kuhakikisha migogoro ya ardhi inatatuliwa na amekuwa mkali kwa maofisa ardhi wa halmashauri ambapo baadhi yao wamebadilishwa vituo kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.

Pamoja na mafanikio hayo, bado kuna watumishi walio chini ya wizara hiyo wanaoendelea kuchafua rekodi ya Lukuvi na kufifisha ndoto za Rais Dk. Magufuli ambaye aliwahi kusema hataki kukutana na kero ya ardhi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Binafsi nimelazimika kuandika andiko hili kutokana na mkazi mmoja wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Milalu Samara, ambaye alifika katika ofisi za gazeti hili akiwa na lundo la nakala mbalimbali akilalamikia kuhangaika kutafuta haki yake kwa miaka minne mfululizo lakini suala lake linaonekana kukwamishwa na baadhi ya watumishi walio chini ya Wizara ya Ardhi.

Namuomba Waziri Lukuvi kutambua bado ana jukumu la kuaangalia uwajibikaji wa watumishi wake katika sekta ya ardhi ngazi ya kanda, mkoa na  wilaya kwani wapo wachache wanaochochea migogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles