25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WANAOFUTA BAADA YA  MESSI NA RONALDO BALLON DOR

ADAM MKWEPU NA MITANDAO


MAISHA ya kuwa katika mbio za kuwania tuzo ya uchezaji bora wa dunia kwa nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Barcelona Lionel Messi huenda  yakawa yanaelekea ukingoni.

Nyota hao sasa wanalingana katika kunyakuwa tuzo hiyo kwa kila mmoja kunyakuwa mara tano baada ya hivi karibuni Ronaldo kushinda  tuzo ya Ballon d’Or 2017.

“Katika miaka michache ijayo natarajia kuchezaji katika kiwango bora,”anasema Ronaldo baada ya kupokea tuzo hiyo.

Akizungumzia Messi, nyota huyo anasema kwamba: “Acha mapambano yaendelee katika njia nzuri, atafanya kwa ubora wake kwa klabu yake pamoja na timu yake ya taifa.

“Nitacheza kwa ubora wangu nikiwa Real Madrid  na timu yangu ya taifa, acha tuone mwisho wa siku nani ni bora zaidi ya mwingine  ambapo atatwaa tuzo hiyo mwisho wa mwaka baada ya watu kupiga kura.”

Ronaldo anasema kwamba anapata faraja kupata mafanikio hayo  akiwa kwenye kazi yake na angependa kushinda kila mwaka.

Nyota huyo  mwenye umri wa miaka (32) alichagulia  akitokea  kwenye orodha ya wachezaji 29 ambao wamepigiwa kura na makundi ya waandishi wa habari 173. Messi  mwenye umri wa maika (30) alimaliza nafasi  ya pili nyuma ya Ronaldo.

Nyota hao kwa sasa wanaonekana kubakisha muda mchache katika vita yao ambayo  imedumu miaka saba.

Neymar, ambaye amejiunga   na klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa Agosti mwaka huu akitokea Barcelona kwa pauni milioni 198 amekuwa nafasi ya tatu katika kinyanyiro hicho huku kipa wa Juventus Gianluigi Buffon akishikilia nafasi ya nne.

Neymar ni wazi kwamba yeye ndio chaguo namba moja baada ya  Ronaldo na Messi. Mbrazili huyo alimaliza nafasi ya tatu 2015 na wa tano mwaka jana kabla ya kurejea tatu bora 2017, hayupo tena chini ya kivuli cha Messi ndani ya Barcelona, baada ya uhamisho wa rekodi ya dunia kwenda PSG  ili kuweza kupata mafanikio binafsi.

Kwenda nje ya Hispania kutamfanya kuwa thabiti kushinda tuzo hiyo hata kama Ligue 1 inaonekana kuwa dhaifu dhidi ya La Liga.

Kinda mahiri wa PSG Kylian Mbappe alimaliza nafasi ya saba katika tuzo hiyo. Mfaransa huyo alitangazwa hivi karibuni kuwa mchezaji bora chipukizi msimu wa 2016/17.

Mbappe aliibuka kwa kasi msimu uliopita aking’ara akiwa na Monaco na kwa haraka akahamia jiji kuu la Ufaransa, Paris alikojiunga na watawala hao wa League 1. Alikiri mwezi Oktoba kuwa bado ana njia ndefu ili kuwa mshindani wa Ballon d’Or, lakini mchezaji huyo mwenye kipaji ana muda mrefu kuliko majina yote yaliyoorodheshwa na wala si kwa Messi na Ronaldo tu.

Mchezaji mwingine anayetarajiwa kufanya makubwa  katika tuzo hiyo baadae ni nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye anang’ara kwenye Ligi Kuu England akiwa na Chelsea, akiisaidia klabu hiyo kutwaa taji hilo mara mbili na pia kutajwa kwenye kikosi cha mwaka cha PFA mara nne katika misimu yake mitano  England. Hata hivyo kwa ubora wake wote ndani ya fulana ya bluu, Mbelgiji huyo ameshindwa kuwashawishi wapiga kura wa Ballon. Akiendelea kuhusishwa na tetesi za kutua Real Madrid mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anaamini hisia kuwa kutua Hispania kutazidi kuipandisha heshima yake kwenye soka.

Nyota wa Juventus, Paulo Dybala,  akiwa mchezaji muhimu  katika timu hiyo  kwa sasa, tumaini lake la Ballon d’Or kwa muda mrefu linaweza kutimia atakapoirithi nafasi ya Messi kwenye timu ya Argentina. Bado umri wake ni miaka 24 na hakuna sababu ya kupata hofu. Ameisaidia Binaconeri kutinga fainali Ligi ya Mabingwa msimu uliopita jambo lililompatia sifa na kukuza wasifu wake, na ameanza kampeni ya Serie A kwa magoli 10 kwenye mechi sita. Ikiwa ataendeleza mwendo huo kwa kipindi kirefu, wapiga kura watalazimika kuanza kumpigia kura.

Mkali mwingine ni nyota wa Manchester City, Kevin De Bruyne,  ambaye katika mbio hizo unaweza kuathiriwa na ukosefu wa ufungaji wa mabao. Utawala wa nyota wakuu wawili Messi na Ronaldo umeimarishwa na umahiri wao wa kufunga – na kuwatengenezea wengine nafasi ya kufunga, lakini kufunga kwenye timu yenye mafanikio kunaongeza sifa. Angalau Mbelgiji huyo yupo kwenye klabu yenye mwelekeo thabiti kwani Manchester City inaweza kuwa klabu yenye nguvu zaidi chini ya uongozi wa Pep Guardiola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles