Imechapishwa: Fri, Aug 11th, 2017

WANANCHI WATAKIWA KUENDELEA KUMWOMBEA JPM

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

VIONGOZI na waumini wa dini mbalimbali nchini, wameshauriwa kuendelea kumwombea Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kutekeleza majukumu kwa faida ya Watanzania.

Ushauri huo umetolewa juzi na Askofu Mkuu wa Kanisa la Maombezi Tanzania, Living Mwambapa, alipokuwa akihubiri kwenye ibada maalumu ya kumshukuru Mungu, iliyofanyika Itega Kikuyu, mjini hapa.

Askofu Mwambapa alisema kwamba, katika kipindi hiki ambacho Rais Dk. Magufuli amefanya kazi ya kutetea rasilimali za nchi, lazima maadui wataongezeka wakiwamo wasiopenda juhudi hizo zifanikiwe.

“Ni vema sisi kama viongozi wa dini na waumini wetu, tumwombee rais wetu ili apate ujasiri na nguvu zaidi katika vita hii.

“Waumini wa madhehebu ya dini hakikisheni mnatumia fursa zilizojitokeza hapa Dodoma baada ya makao makuu kuhamia hapa.

“Ni muda mrefu wakazi wa Dodoma wamekuwa wakiahidiwa kuwa Serikali itahamia Dodoma na sasa imehamia kweli. Kwa hiyo wananchi wasibweteke na badala yake watumie fursa zilizopo katika kujiinua kiuchumi,” alisema Askofu Mwambapa.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

WANANCHI WATAKIWA KUENDELEA KUMWOMBEA JPM