28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wamkataa mwenyekiti wao

mtz2

NA ELIUD NGONDO, RUNGWE

WAKAZI wa Kitongoji cha Tembela, kilichopo Kijiji cha Mbeye One, Kata ya Isongole, Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya, wamemkataa Mwenyekiti wao, Paskali Japheti, wakimtuhumu kutumia vibaya fedha za maendeleo.

Tukio hilo lilitokea katika kitongoji hicho juzi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwa ajili ya kujadili suala la maendeleo.

Pamoja na kumtuhumu kiongozi wao huyo kutafuna fedha, wananchi hao walishindwa kueleza kiasi halisi cha fedha zilizotafunwa ingawa walisema ni fedha nyingi.

Mmoja wa wananchi hao, Musa Mwakatwila, alisema, baada ya tuhuma kuzidi, mwenyekiti huyo aliandika barua ya kuachia ngazi ingawa hakueleza fedha anazotuhumiwa kuzitafuna atazirudishaje.

“Sisi tunataka atusomee kwanza mapato na matumizi ya fedha zetu, baadaye ajiuzulu na siyo kujiuzulu kwa barua wakati anajua kuna maswali anatakiwa kujibu.

“Anajiuzulu wakati anajua amekuwa akikusanya fedha za michango mbalimbali kwa ajili ya maendeleo na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi,” alisema Mwakatwila.

Wakati wananchi wakitoa shutuma hizo, Japhet alisimama na kusema hajawahi kuandika barua ya kujiuzulu na kwamba bado yeye ni mwenyekiti halali wa kitongoji hicho.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Ikumbaga Mwantela, alisema matumizi ya fedha hizo zinatakiwa kutolewa ufafanuzi kwa kuwa wananchi huzichanga kwa ajili ya maendeleo yao.

“Huyu jamaa ni mtu wa ajabu sana, aliwahi kutangaza kwamba amejiuzulu katika mkutano wa hadhara, lakini leo anasema hajawahi kujiuzulu,” alisema.

Wakati mwenyekiti huyo akiendelea kuzungumza, wananchi walianza kupiga kelele wakitaka fedha zao zilizotafunwa zirudishwe hali iliyosababisha Diwani wa Kata ya Isongole, Lawrence Mfwango, aingilie kati na kusema atapeleka suala hilo wilayani ili likafanyiwe kazi.

“Kuweni watulivu, nitapeleka malalamiko yenu wilayani na Julai 19, nitakuja na viongozi wa wilaya wawapatie mrejesho na siku hiyo ndiyo uamuzi utafanyika hapa hapa,” alisema diwani huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles