27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

WANANCHI WAKATAA VYANDARUA VYA SERIKALI

Na ASHURA KAZINJA, MOROGORO


BAADHI ya wananchi mkoani Morogoro, hawatumii vyandarua vinavyotolewa na Serikali kwa madai kwamba vinapunguza nguvu za kiume.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo  wa Kikundi cha Ngoma Afrika Morogoro, Maya Devie, alipokuwa akizungumza mjini hapa.

Kutokana na hali hiyo, Devie alisema kikundi chao kimechukua jukumu la kutoa elimu kwa wananchi ili watumie vyandarua hivyo kwa kuwa havina madhara yoyote kwa afya ya binadamu.

“Elimu hiyo ya malaria tumekuwa tukiitoa kwa njia ya sanaa kwa sababu tusipofanya hivyo, wananchi wataendelea kuathiriwa na maradhi hayo kila wakati.

“Tumelazimika kuchukua uamuzi huo kwa sababu baadhi ya wananchi wanatumia vyandarua hivyo kufugia kuku na kuvulia samaki kwenye mito badala ya kuvitumia kujikinga na maralia kwa sababu wanasema eti vinapunguza nguvu za kiume.

“Kwa kuwa watu wengi wanapenda sanaa, tunalazimika kuchomekea na mafundisho ya madhara ya maralia katika jamii pamoja ili wananchi wengi waachane na mila hizo potofu na kuanza kutumia malaria,” alisema Devie.

Kwa upande wake, Mratibu wa Malaria Manispaa ya Morogoro, Dk. Ernest Rugiga, alisema licha ya kuwapo kwa changamoto katika matumzi ya vyandarua, kiwango cha maambukizi kimeshuka hadi kufikia asilimia saba mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 38 za mwaka 2015.

“Bado tunazidi kuwasisitiza wananchi watumie vyandarua vinavyotolewa na Serikali kwa sababu havina madhara kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

“Nawaomba wananchi wasisikilize maneno ya watu wasiokuwa na utaalamu wa tiba, bali waisikilize Serikali kwa sababu haiwezi kuwaletea vitu vinavyoathiri afya zao,” alisema Dk. Rugiga.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles